BOBI WINE AKATISHA MAHOJIANO YAKE NA RADIO

#FAHAMU Mgombea wa Urais nchini Uganda Robert Kyagulanyi amelazimika kukatiza mahojiano yake na radio baada ya wanajeshi kuvamia nyumba yake mjini Kampala"

Vyombo vya habari nchini Uganda vinaripoti kuwa leo asubuhi wanajeshi waliizingira nyumba yake , na kuwakamata walinzi wake wote na mtu yeyote waliyempata katika eneo la makazi ya mwanasiasa huyo wa upinzani Hata hivyo hakuna sababu iliyotolewa juu ya uvamizi huo"

Wakati haya yakijiri Rais Yoweri Museveni ambaye anawania muhula wa sita madarakani anatarajiwa kulihutubia taifa leo kupitia vyombo vya habari vya kitaifa. Waganda wanatarajia kufanya uchaguzi wa wabunge na rais siku ya Alhamisi"

Kampeni za uchaguzi nchini uganda zimekuwa zikigubikwa na gasia zilizosababisha mauaji."
#BinagoUPDATES 

No comments