amka na Bwana
🌾🌾🌾🌾🌾🌾🌾🌾🌾🌾
*KESHA LA ASUBUHI*
*JUMATATU, SEPTEMBA 7,2020*
SOMO: *MAISHA YA DANIELI YA KIASI*
*Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kamwe kwa chakula cha Mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi*
Danieli 1 : 8
📝Maisha ya Danieli ni kielelezo chenye maongozi ya Mungu juu ya kile kinachounda tabia iliyotakaswa. Hutoa fundisho kwa wote, hasa kwa vijana. Kufuata kwa umakini mkubwa maelekezo ya Mungu huleta manufaa kwa afya ya mwili na akili.
📝Ili kufikia viwango vya juu kabisa vya maadili na akili, ni muhimu kutafuta hekima na nguvu kutoka kwa Mungu na kuzingatia hasa kiasi katika tabia zote za maisha. Katika uzoefu wa Danieli na rafiki zake tuna mfano wa ushindi wa kanuni dhidi ya kuendekeza uchu wa chakula. Inaonesha kwamba kupitia kanuni za kidini vijana wanaweza kushinda tamaa za mwili, na kubaki waaminifu kwa masharti ya Mungu, hata kama inawagharimu kujikana kwa kiasi kikubwa mno.
📝Danieli alikuwa mtumishi wa Mungu Aliye juu aliyejitoa kikamilifu. Maisha yake marefu yalijawa na matendo mema ya huduma kwa Bwana wake. Tabia yake safi kabisa na uaminifu wake usioyumba inalandana na unyenyekevu wake wa moyo na toba kamili mbele za Mungu. Tunarudia tena, maisha ya Danieli ni kielelezo chenye maongozi ya Mungu kuhusu utakaso wa kweli.
📝Popote pale wanapoweza kuwa, wale waliotakaswa kikamilifu watakuza viwango vyao vya maadili kwa kutunza kwausahihi kanuni za afya, na kama Danieli, kuonesha wengine mifano ya kiasi na kujikana nafsi .... Ni kwa umakini kiasi gani Wakristo wanapaswa kudhibiti tabia zao, ili waweze kuhifadhi nguvu kamili za kila nyanja kwa ajili ya huduma kwa Kristo.
📝Wale wanaohifadhi kwa upendo mkubwa nuru ambayo Mungu ameitoa juu ya matengenezo ya afya wana msaada muhimu katika kazi ya kutakaswa kupitia kweli na kuandaliwa kwa ajili ya kuvaa kutokufa.
*_TAFAKARI NJEMA_*
🌲🌲🌲🌲🌲🌲🌲🌲🌲
Post a Comment