amka na Bwana
#KESHA_LA_ASUBUHI
JUMANNE, SEPTEMBA 8
SOMO: *MAISHA YA UTAKATIFU YA HENOKO*
*_Henoko akaenda pamoja na Mungu… miaka mia tatu Mwanzo 5 : 22_*
➡️🙏🏾Kulikuwa na safu ya watu watakatifu, waliokuzwa na kuadilishwa kwa muunganiko na Mungu, waliishi kama waliokuwa pamoja na jamii ya mbinguni. Walikuwa watu wenye akili sana, na mafanikio ya kustaajabisha. Walikuwa na ujumbe mkuu na mtakatifu kujenga tabia ya haki, kufundisha somo la utauwa, sio kwa watu wa kipindi chao tu, lakini pia vizazi Vijavyo.
👉🏿Kuhusu Henoko imeandikwa kuwa aliishi miaka sitini na tano, na akapata mtoto mwanamume. Baada ya hapo alitembea pamoja na Mungu kwa miaka mia tatu. Kwa miaka hiyo ya mwanzo, Henoko alikuwa amempenda na kumcha Mungu na kutunza amri zake. Kutoka kwa kinywa cha Adamu alikuwa amejifunza kisa cha kusikitisha juu ya anguko na kisa cha kufurahisha cha neema ya Mungu kama ilivyooneshwa katika ahadi, na alimtumainia Mkombozi aliyekuwa akitarajiwa.
🙏🏾Lakini baada ya kuzaliwa mwanawe wa kwanza Henoko alifikia uzoefu wa juu zaidi: alivutwa kuingia katika uhusiano wa karibu zaidi na Mungu. Alielewa vyema zaidi wajibu na majukumu yake kama mtoto wa Mungu. Na kadiri alivyoona upendo wa mtoto kwa baba yake, tumaini lake sahili kwa ulinzi wake, alipohisi shauku ya moyo wa kina kwa mzaliwa wake wa kwanza, alijifunza somo la pekee 1a upendo wa kustajabisha wa Mungu kwa wanadamu kupitia zawadi ya Mwana wake na imani ambayo watoto wa Mungu wanapaswa kuweka kwa Baba yao wa mbinguni.
💜Upendo wa Mungu usio na ukomo, usiochunguzika kupitia kwa Kristo ulikuwa tafakari yake usiku na mchana, na kwa bidii yote ya nafsi yake aliazimu kuufunua upendo huo kwa watu ambao aliokaa kati yao. Kutembea pamoja na Mungu kwa Henoko hakukuwa kwa kuzubaa au maono, bali katika kila wajibu wa maisha yake.... Katika familia yake na mahusiano na wengine, kama mume na baba, rafiki, raia, alikuwa mtumishi wa Bwana imara asiyeyumba.
*_MUNGU ATUSAIDIE KATIKA KIZAZI CHETU TUSIMAME KAMA HENOKO._*
Post a Comment