mhafahamu Martin Luther

Luther akimtegemea Kristo pekeyake mbele ya mhadhara wa watu mashuhuri sana aliichoma moto amri ya Papa (The Papal bull) na akijawa na nguvu ya Roho wa Mungu alisema "Pambano zito ndio limeanza. Kabla ya hapo nilikuwa tu nacheza na Papa. Nilianza kazi hii kwa jina la Mungu; na itamalizika bila mimi na kwa nguvu zake" Na alipotishwa kwamba atakapohudhuria mahakamani watamchoma moto kama John Huss, Luther alijibu "Hata kama watawasha moto njia nzima kutoka Worms hadi Wittenberg kwa jina Bwana nitatembea kwenye njia hiyo; nitasimama mbele yao nikimkiri Bwana Yesu" na amri ya Papa ilipomfikia Luther alisema "Ninaidharau na kuishambulia kuwa inakufuru na niyauwongo. Ni Kristo mwenyewe aliyeshtumiwa ndani yake. Tayari ninahisi uhuru mkubwa moyoni mwangu maana hatimaye ninafahamu kwamba Papa ni mpinga Kristo na kwamba kiti chake ni kile cha shetani mwenyewe" na akiwa anakaribia kufika huko Worms rafiki zake walihofu huenda atanyongwa lakini mjoli wa Mungu Luther akasema "Hata kama mji wa Worms utakuwa na mashetani wengi kama vigae vya paa la nyumba, bado nitauingia" 

Wengi sana waliokolewa na mchungaji huyu ambaye hakuwa na mshahara hata kidogo. Mchungaji Luther kwa wakati wake alikuwa mtetezi mashuhuri wa biblia peke yake kiasi kwamba alikuwa tayari kufa kwa kuzitetea kanuni nyoofu za biblia takatifu 
 Ellen G. White, Tumaini Kuu. Uk 78-111
D'Aubgne, bk 2 chap 2.
K. K Hangenbach. History for reformation, vol 1 pg 96.
Martyn - The life and time of Luther, pp 271272

 Mungu leo anahitaji watu jasiri, watakao simama kuutetea ukweli wa biblia hata mbingu ianguke watakaoitaja dhambi kwa jina pasipo kuogopa yeyote wala chochote...!

Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv

No comments