amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

Jumanne 04/08/2020

*NURU YENU NA IANGAZE*

*Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.* Mathayo 5:14-16

📜 Ikiwa mnatembea katika nuru, kila mmoja wenu anaweza kuwa mbeba nuru kwa ulimwengu. Usitafute kukamilisha kazi fulani kubwa huku ukipuuza fursa ndogo ndogo zilizo karibu. Tunaweza kufanya mengi kwa kuonesha mfano wa ukweli katika maisha yetu ya kila siku. 

📜 Mvuto ambao tunaweza kuuweka kwa jinsi hiyo hauwezi kupingwa kwa urahisi. Watu wanaweza kupambana na kudharau mantiki yetu; wanaweza kupinga miito yetu; lakini maisha yenye kusudi takatifu, yenye upendo usio na upendeleo kwa niaba yao, ni hoja iliyo upande wa ukweli ambayo hawawezi kuikana. 

📜 Mengi zaidi yanaweza kufanikishwa kwa maisha ya unyenyekevu, ya kujitolea, na ya wema kuliko yanavyoweza kuguswa na mahubiri ambayo ndani yake mfano wa uchaji wa Mungu unakosekana. Unaweza kujitahidi kujenga kanisa, kuwatia moyo ndugu zako, na kufanya mikutano ya kijamii kuvutia; na unaweza kuruhusu sala zako kwenda nje, kama miundu mikali, pamoja na wafanyakazi kwenye uwanja wa mavuno. Kila mmoja anapaswa kuwa na shauku binafsi, mzigo juu ya roho, kukesha na kuomba kwa ajili ya mafanikio ya kazi. 

📜 Unaweza pia kwa upole kuwavuta wengine katika ukweli wa Neno la Mungu. Vijana huenda wasiweze kutoa ukweli kutokea mezani, lakini wangeliweza kwenda nyumba kwa nyumba na kuwaelekeza watu kwa Mwanakondoo wa Mungu achukuaye dhambi ya ulimwengu. Vumbi na takataka za makosa zimefunika Vito vya thamani vya ukweli; lakini wafanyakazi wa Bwana wanaweza kufunua hazina hizi, ili watu wengi wapate kuziangalia kwa furaha na kicho. 

🔘 *Kuna aina mbalimbali za kazi, zilizorekebishwa kwa ajili ya akili na uwezo anuwai. Katika siku ya Mungu hakuna atakayesamehewa kwa kujifungia kwake katika maslahi yake ya ubinafsi. Na ni kufanya kazi kwa ajili ya wengine ndiko kutakakohifadhi mioyo yenu wenyewe kuwa hai.... Juhudi ya dhati, isiyo na ubinafsi itakusanya miganda kwa Yesu.... Bwana ni msaidizi mwenye nguvu.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv

No comments