kuachwa na umpendae

UKIACHWA NA UMPENDAE, MSHUKURU MUNGU NA ANZA MAISHA YAKO UPYA:

Miongoni mwa Mambo ambayo huwa na ugumu katika kuyavulimia ikiwa yametokea katika Maisha ya mtu ni pale ambapo mtu anapoachwa kwa namna yoyote na yule ampendae.

Linapo tokea Jambo la kuachwa lazima ukubaliane na Matokeo maana upo msemo usemao "Nyani mzee hafundishwi kanuni mpya". 

Ukishindwa kukubaliana na kuachwa na umpendae unaweza kuishi maisha ya mateso kwa sababu ya kutokuelewa ule msemo usemao, "Asiyekwenda asikucheleweshe".

Unapoachwa na umpendae lazima ukubali na kumshukuru Mungu kwa hatua hiyo ya kuachwa maana unapoachwa bila sababu ni wazi kuwa utaishi katika msemo usemao "Akutazamae sana hukufundisha namna ya kuvaa vizuri".

Mshukuru Mungu kwa sababu ya kuachwa na ufungue mlango upya wa maisha yako ili upate kuishi maisha ambayo hayatakuwa na masononeko ya kudumu, maana upo msemo usemao "Kuku mwenye mguu mmoja hawezi kuwa na mbio kama kuku mwenye miguu yote"

Anza sasa maisha yako upya, usiishi kwa kutegemea kivuli kisicho na msaada wowote kwako. Kuendelea kuzimba mbingu isitoe mvua ni kupoteza muda.

ASANTE.
The Light Of Universe Ministry
Mwl Ejide Andrew Noah
+255743154575.

No comments