amka na Bwana

*KESHA LA ASUBUHI*

JUMANNE; AGOSTI 11, 2020

SOMO: *WAPE WANAUME NA WANAWAKE MAJI YA UZIMA*

*Walakini yeyote atakaye kunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.*
Yohana 4:14

✍️Katika mazungumzo yake na mwanamke Msamaria, badala ya kukishusha hadhi kisima cha Yakobo, Kristo aliwasilisha kitu kilicho bora.... Aligeuza mazungumzo hayo kwenda katika hazina ambayo alitazamia kuitoa, akiahidi kumpa mwanamke yule kitu bora kuliko kile alichokuwa nacho, yaani maji yaliyo hai, furaha na tumaini la injili. 

 ✍️Ni shauku kubwa kiasi gani Kristo alidhihirisha kwa mwanamke huyu! Jinsi gani maneno yake yalikuwa ya kweli na fasaha! Mwanamke huyo alipoyasikia, aliacha mtungi wake wa maji na akaenda mjini, akiwaambia wale aliokutana nao, Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo? 

✍️ Tunasoma kwamba Wasamaria wengi wa mji ule walimwamini. Na ni nani anayeweza kukisia mvuto ambao maneno haya yameweka kwa ajili ya uokoaji wa roho katika miaka iliyofuatia tangu wakati ule! 

 ✍️Yesu aliwasiliana na watu kila mmoja binafsi. Hakujitenga na kukaa mbali na watu wale waliohitaji msaada wake. Aliingia katika maskani ya watu, akafariji waombolezaji, akawaponya wagonjwa, akawatia nguvu wazembe, akaenda huko na huko akitenda mema. Na ikiwa tutafuata nyayo za Yesu, lazima tufanye kama alivyofanya. Lazima tuwapatie watu aina ile ile ya msaada aliyoitoa. 

 ✍️Bwana anatamani kwamba neno lake la neema lifikishwe kwa kila roho. Kwa kiwango kikubwa hili itabidi litimizwe na kazi ya mtu binafsi. Hii ndio ilikuwa mbinu ya Kristo. Kazi-yake kwa sehemu kubwa ilihusisha mahojiano na watu binafsi. Aliheshimu kwa dhati hadhira ya roho moja. Kupitia kwa roho hiyo moja ujumbe mara nyingi ulienezwa kwa maelfu.... Kuna watu wengi ambao kamwe hawatafikiwa na injili isipokuwa imepelekwa pale walipo.

*ASUBUHI YA LEO IKAWE YA BARAKA TELE.... TAFAKARI NJEMA MPENDWA*

No comments