amka na Bwana
#KESHA_LA_ASUBUHI
JUMATANO, AGOSTI 19
SOMO: *UWE MWENYE FADHILI NA MWENYE HURUMA*
*_💜Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi." (Waefeso 4:32)_*
🙏🏾Hebu huruma na fadhili ambazo Yesu amefunua katika maisha Yake ya thamani kubwa ziwe mfano kwetu kwa jinsi tunavyopaswa kuwatendea wanadamu wenzetu.... Wengi wamenyong'onyea na kukata tamaa katika mapambano makuu ya maisha, ambao neno moja tu la wema la kuchangamsha na kutia moyo lingeweza kuwaimarisha na kuwafanya waweze kushinda....
🙏🏾Sisi hatuwezi kujua athari nyingi zinazoweza kuletwa na maneno yetu laini ya fadhili, juhudi zetu kama za Kristo katika kupunguza uzito wa mzigo fulani. Wakosaji hawawezi kurejeshwa kwa njia nyingine yoyote isipokuwa kwa roho ya unyenyekevu, upole, na upendo.
🙏🏾Katika kushughulika kwako kote na wanadamu wenzako kamwe usisahau kuwa unashughulika na mali ya Mungu. Kuwa mwenye fadhili; kuwa mwenye huruma; kuwa mwenye adabu. Heshimu milki ambayo imenunuliwa na Mungu. Tendeaneni kwa huruma na adabu.
🙏🏾Ikiwa una uadui, Shaka, husuda, na wivu mioyoni mwenu, basi mna kazi ya kufanya ili kuyarekebisha mambo haya. Ungameni dhambi zenu; mpate kuelewana na ndugu zenu. Zungumza mema juu yao. Usitoe Vidokezo vyovyote Visivyofaa, ambavyo vitaamsha shuku katika akili za wengine. Linda sifa zao kwa heshima sana kama vile ambavyo ungetaka wailinde ya kwako; wapende kama ambavyo ungelitaka upendwe na Yesu.
🙏🏾Neema ya Mungu huwaongoza watu katika shughuli zao zote za biashara kujiweka mahali pa wale ambao wanashughulika nao. Inawaongoza watu kutokuangalia mambo yao wenyewe bali pia mambo vya wengine. Inawaongoza katika kudhihirisha upole, huruma, na wema. Kuhifadhi roho sahihi kwa upendo mkuu, kuishi maisha matakatifu-huku ndiko kuwa kama Kristo kunamaanisha .... Hebu maisha yako yatawaliwe na kanuni pana, za ukarimu za Biblia, kanuni za mapenzi mema, fadhili, na uungwana.
*_🙏🏾ROHO MTAKATIFU ATUGUSE KILA MMOJA WETU ILI KUTAMBUA DHAMBI ZETU NA KUZIUNGAMA KWA JINA LA YESU. AMINA._*
Post a Comment