Amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

Alhamisi 27/08/2020

*UWE MACHO KWA KIPOFU; MIGUU KWA VILEMA*

*Nalikuwa macho kwa kipofu, Nalikuwa miguu kwa aliyechechemea.* Ayubu 29:15

💎 Angalia kwa uangalifu, kwa maombi, kwa bidii, akili isije ikashughulishwa sana na shughuli nyingi muhimu za biashara kiasi kwamba uchaji Mungu wa kweli unapuuzwa na upendo kuondolewa kutoka rohoni, licha ya hitaji kubwa na la kusikitisha la wewe kuwa mkono wa msaada kwa Mungu kwa ajili ya vipofu na kwa watu wengine wote walio maskini. 

💎 Wale ambao hawana marafiki kabisa wanahitaji kuzingatiwa zaidi. Tumia muda wako na nguvu kujifunza jinsi ya kuwa na juhudi katika roho, huku ukishughulika kwa haki, na kupenda rehema, mkimtumikia Bwana. Kumbuka kwamba Kristo anasema, Kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. 

💎 Mungu anataka watu wake wawe na huruma na wenye kuwafikiria zaidi wale walio maskini kuliko wao walivyo.... Mungu anataka kuwa huruma ile ile ambayo anaoneshwa mjane na yatima waoneshwe pia kipofu na wale wanaosumbuka kwa mateso mengine ya udhaifu wa kimwili. 

💎 Ukarimu usio na upendeleo ni adimu sana katika zama hizi za ulimwengu.... Inashangaza kwamba watu wanaokiri kuwa Wakristo wanapuuza mafundisho ya wazi, yaliyo chanya ya Neno la Mungu bila hata kuhisi majuto ya dhamiri. Mungu anaweka juu yao jukumu la kuwajali maskini, vipofu, Vilema, mjane, na yatima; lakini wengi hawafanyi bidii kuizingatia hili. 

🔘 *Kuna kazi kubwa inayopaswa kufanywa katika ulimwengu wetu, na kukaribia mwisho wa historia ya dunia, hakuipunguzi hata kwa kiwango kidogo; lakini upendo mkamilifu wa Mungu unapokaa moyoni, mambo ya ajabu yatatendwa.*

*TAFAKARI NJEMA SANA*👮‍♂️

Je una taarifa ya kusisimua kuhusu dini unataka tuchapishe,tafadhali tuma kupitia whatspp +255759701713

No comments