amka na Bwana
*KESHA LA ASUBUHI.*
Jumapili 23 Agosti 2020.
*WATEMBELEE YATIMA NA WAJANE.*
*Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa. Yakobo 1:27.*
▶️Miongoni mwa wote ambao mahitaji yao yanataka usikivu wetu, mjane na yatima wana madai yenye nguvu kubwa kabisa juu ya huruma na utunzaji wetu.... Baba ambaye amekufa katika imani, akitegemea ahadi ya milele ya Mungu, aliwaacha wapendwa wake akiwa na imani kamili kwamba Bwana atawatunza. Je! ni jinsi gani Bwana anawakimu hawa waliofiwa?
▶️Hafanyi muujiza wa kutuma mana kutoka mbinguni, hatumi kunguru kuwaletea chakula; bali anafanya muujiza kwenye mioyo ya wanadamu, Anafukuzia mbali ubinafsi kutoka rohoni, anafungua chemchemi ya ukarimu. Hujaribu upendo wa wanaokiri kuwa wafuasi wake kwa kuwaweka chini ya ufadhili wao wale wanaoteseka na waliofiwa, maskini na yatima.
▶️Kina mama wengi wajane pamoja na watoto wao wasio na baba wanahangaika kwa ushujaa kubeba mzigo wao ulio mara dufu, mara nyingi akifanya kazi kuzidi sana nguvu zake ili kuwaweka wale walio wadogo karibu yake na kuwapa mahitaji yao. Ana muda mdogo kwa ajili ya mafunzo yao na maelekezo kwao, fursa ndogo ya kuwazingira kwa mivuto ambayo ingelichangamsha maisha yao. Anahitaji kutiwa moyo, huruma, na msaada halisi. Mungu anatuita tupate kuwapa watoto hawa, kadiri tuwezavyo, hitaji la huduma ya baba.... .Jitahidi kumsaidia mama huyu aliyechakazwa kwa matatizo.
▶️Katika nyumba zenye hali njema za maisha, katika mapipa ya kuhifadhia nafaka na maghala ya nafaka yaliyojazwa na mazao ya mavuno tele, katika mabohari yalimohifadhiwa bidhaa za kufumwa, na ghala za chini zilimohifadhiwa dhahabu na fedha, Mungu ametoa uwezo wa kutoa riziki kwa hawa wahitaji.
▶️Wale ambao huwahurumia wajane, mayatima, na wahitaji, Kristo anawawasilisha kama watunza amri, ambao watapata uzima wa milele.
*MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE.*
🙏🙏🙏🙏
Post a Comment