amka na Bwana

#KESHA_LA_ASUBUHI
🥗🥗🥗🥗🥗🥗🥗🥗

IJUMAA, AGOSTI 21

SOMO: *UWE MWENYE HURUMA NYINGI*

*_💜Nuru huwazukia wenye adili gizani; Anafadhili na huruma na haki. Zaburi 112:4_*

Mahali popote panapokuwapo msukumo wa upendo na huruma, popote ambapo moyo unapofikia ili kuwabariki na kuwainua wengine, panadhihirishwa kazi ya Roho Mtakatifu wa Mungu. 

 Katika Vina virefu vya upagani watu ambao hawajapata maarifa ya sheria ya Mungu iliyoandikwa, ambao hata kamwe hawajawahi kusikia jina la Kristo, wamekuwa wema kwa watumwa Wake, wakiwalinda huku wakihatarisha maisha yao wao wenyewe. Matendo yao yanaonesha utendaji wa nguvu ya Mungu. Roho Mtakatifu ametia neema ya Kristo ndani ya moyo wa mtu katili asiyestaarabika, ikihuisha huruma zake kinyume na tabia yake, kinyume na elimu yake.... 

 Kristo anatafuta kuwatia moyo wale wote ambao watainuliwa kufanya ushirika na Yeye mwenyewe, ili tupate kuwa wamoja pamoja naye kama vile Yeye alivyo umoja pamoja na Baba. Anaturuhusu tukutane na mateso na msiba ili kutuita kutoka kwenye ubinafsi wetu; Anajitahidi kukuza ndani yetu sifa za tabia Yake-huruma, upole, na upendo. Kwa kuikubali kazi hii ya huduma tunajiweka wenyewe katika Shule yake, ili tuandaliwe kwa ajili ya nyua za Mungu.... 

 Kwa kushirikiana na viumbe vya mbinguni katika kazi yao hapa duniani, tunajiandaa kwa ajili ya ushirika pamoja nao kule mbinguni. Roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu, malaika mbinguni watawakaribisha wale ambao duniani wameishi sio kutumikiwa, bali kutumika. Katika ushirika huu uliobarikiwa tutajifunza, kwa furaha yetu ya milele, yote ambayo yamefungwa katika swali, Jirani yangu ni nani? 

 Kila tendo la upendo, kila neno la wema, kila sala kwa niaba ya anayeteseka na kudhulumiwa, inaripotiwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na kuwekwa katika kumbukumbu isiyoweza kuharibika ya mbinguni.

*_TAFAKARI NJEMA, MAANDALII IWE NJEMA PIA.🙏🏾_*

No comments