amka na Bwana
#KESHA_LA_ASUBUHI
ALHAMISI, AGOSTI 20
SOMO: *UWE NA MOYO WENYE UELEWA*
*_Nimekupa moyo wa hekima na wa akili. 1 Wafalme 3: 12_*
Sulemani katika ujana wake alifanya chaguo la Daudi kuwa lake mwenyewe. Zaidi ya mazuri yote ya kidunia aliomba kwa Mungu moyo wenye hekima na akili.... Uwezo wake wa ufahamu, kiwango cha maarifa yake, utukufu wa utawala wake, vilitokea kuwa maajabu ya dunia.
Jina la Yehova liliheshimiwa sana wakati wa sehemu ya kwanza ya utawala wa Sulemani. Hekima na haki iliyodhihirishwa na mfalme ilishuhudia kwa mataifa yote juu ya ubora wa sifa za Mungu aliyemtumikia. Kwa muda fulani Israeli ilikuwa kama nuru ya ulimwengu, inayoonesha ukuu wa Yehova.
Sio katika hekima inayozidi, utajiri wa ajabu, nguvu na umaarufu wake ambavyo vilikuwa na athari nyingi, kwamba ndimo ulimokuwamo utukufu halisi wa utawala wa awali wa Sulemani; bali katika heshima ambayo yeye aliileta kwa jina la Mungu wa Israeli kupitia matumizi ya busara ya zawadi za Mbingu.
Kadiri miaka ilivyopita na sifa za Sulemani kuongezeka, alijitahidi kumtukuza Mungu kwa kuzidisha nguvu zake za kiakili na za kiroho na kwa kuendelea kutoa kwa wengine baraka alizozipokea. Hakuna aliyeelewa vyema zaidi kuliko yeye kwamba ilikuwa ni kupitia kwa fadhila ya Yehova ndipo alipopata umiliki wa nguvu na hekima na akili, na kwamba zawadi hizi zilitolewa ili apate kutoa kwa ulimwengu maarifa ya kumfahamu Mfalme wa wafalme.
Kadiri mtu anapoongolewa na ukweli, kazi ya matengenezo ya tabia inaendelea. Anakuwa na kiwango cha nyongeza cha ufahamu, katika kuwa mtu wa kumtii Mungu. Akili na mapenzi ya Mungu yanakuwa ndio mapenzi yake, na kwa kumtegemea Mungu daima kwa ajili ya ushauri, anakuwa mtu mwenye akili iliyozidishwa. Kuna ukuzaji wa jumla wa akili ambao umewekwa chini uongozi wa Roho wa Mungu peke yake.
*_BARIKIWA NA BWANA UNAPOTAFAKARI KESHA LA ASUBUHI._*
Post a Comment