amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

JUMATATU, AGOSTI 10, 2020

 *KUWAPA AHUENI WANADAMU WANAOTESEKA* 

 *Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa.* 
Luka 9:2

📄Kristo alianzisha hospitali yake ya muda kwenye miteremko ya vilima vya kijani kibichi vya Galilaya na katika kila mahali pengine ambapo wagonjwa na wenye mateso wangeliweza kuletwa kwake. Katika kila jiji, kila mji, kila kijiji alipopita, kwa huruma ya Baba mwenye upendo Aliweka mkono Wake juu ya walioteseka, na kuwaponya. Kazi hii ndio Kristo amelipa uwezo kanisa lake lipate kuifanya. 

 📄Katika kufunga huduma Yake duniani, wakati Alipowapa wanafunzi Wake agizo kuu "Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe," Alitangaza kwamba huduma yao ingelipata uthibitisho kupitia kwa urejeshwaji wa wagonjwa katika afya njema. Wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, alisema, "nao watapata afya." Marko 16: 15, 18. Kwa kuponya kwa jina lake magonjwa ya mwilini, wangeshuhudia kuhusu uweza wake kwa ajili ya uponyaji wa roho. 

📄 Agizo la Mwokozi kwa wanafunzi wake linawajumuisha waumini wote hadi mwisho wa wakati.... Kamwe haijawahi kutokea haja ya ulimwengu ya mafundisho na uponyaji kuwa kubwa kuliko ilivyo leo hii. Ulimwengu umejaa tele wale wanaohitaji kuhudumiwa-walio dhaifu, wasio na msaada, wajinga, waliodhiliwa. 

📄 Watu wa Mungu wanapaswa kuwa wamisionari wa kweli kwa njia ya matibabu. Wanapaswa kujifunza kuhudumia mahitaji ya roho na ya mwili. Wanapaswa kujua jinsi ya kutoa matibabu ya kawaida ambayo husaidia sana kupunguza maumivu na kuondoa magonjwa. Wanapaswa kufahamu kanuni za matengenezo ya afya, ili waweze kuwaonesha wengine jinsi ambavyo, kwa tabia sahihi ya kula, kunywa, na kuvaa, magonjwa yanaweza kuzuiwa na afya kupatikana tena. Tabibu Mkuu atambariki kila mmoja atakayesonga mbele kwa unyenyekevu na kwa uaminifu, akijitahidi kutoa ukweli wa leo. 

📚 *Kwa maana ya pekee uponyaji wa wagonjwa ni kazi yetu.*


USISAHAU ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv

No comments