amka na Bwana

*LESONI LEO.*

Jumamosi 01 Agosti 2020.

*SOMO: UWEZEKANO USIO NA KIKOMO.*

SABATO MCHANA.

Somo la Juma Hili: 1 Kor. 12:12; Mathayo 3:16, 17; 1 Kor. 12:7; 1 Kor. 1:49, Mathayo 25:14–30.

*Fungu la Kukariri: "Lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye" (1 Wakorintho 12:11).*

Mungu anatuita tushuhudie kwa niaba Yake (Matendo 1:8, Isa. 43:10). Ushuhudiaji siyo karama maalumu ya kiroho ya wateule wachache. Ushuhudiaji ni wito wa Mungu kwa kila Mkristo. Biblia inatumia misemo mbalimbali kuelezea kazi ya ushuhudiaji. Inatupasa kuwa "nuru ya ulimwengu," "mabalozi wa Kristo," na "ukuhani wa kifalme" (Mathayo 5:14, 2 Kor. 5:20, 1 Pet. 2:9). Mungu huyu huyu anayetuita kushuhudia na kuhudumu anatuwezesha kuifanya kazi hiyo. Anagawa karama kwa kila muumini. Mungu hawaiti watu wenye sifa. Anawapa sifa wale anaowaita. Kama vile anavyowapa bure wokovu wanaomwamini, anawapa karama bure pia. 

Tunapojiweka wakfu kwa Mungu na kusalimisha maisha yetu ili kumtumikia, uwezo wetu wa kutumika hauna kikomo. "Hakuna kikomo cha utumishi wa mtu ambaye, anaweka ubinafsi kando, na kumruhusu Roho Mtakatifu afanye kazi katika moyo wake, na anaishi maisha yaliyosalimishwa kikamilifu kwa Mungu." Ellen G. White, The Ministry of Healing, uk. 159. 

Katika somo la juma hili, tutajifunza uwezekano usio na kikomo wa huduma yetu kwa njia ya karama ya Roho Mtakatifu.

*_Jifunze Somo la Juma hili kwa ajili ya Sabato ya Agosti 8._*
🙏🙏🙏🙏

No comments