wanandoa tu!jifunze uokoke

*MUME NA MKE, INASISIMUA SANA..*

Mwanaume kabla ya kuondoka kwenda kazini, aliacha barua juu ya meza ya chakula kwa mkewe,.

Kazi za ndani ya  nyumba yake zilimzuia mwanamke huyo kutokuona barua hiyo hadi saa 12 jioni.

mwishowe alifika kwenye meza hiyo, na  aliona barua juu meza,  alifurahi sana kuona kwamba mumeo alikuwa amepata muda wa kumuandikia barua. 

Aliibusu karatasi hiyo wakati alipoona  neno "mke wangu mrembo"ikiwa imeandikwa juu ya barua hiyo, kisha akaikumbatia alipoona maandishi aliyosomeka "nakupenda kwa moyo wangu wote" mwisho wa barua  na kuinusa na aligundua ilikuwa harufu nzuri ya manukato ya mumewe.

Kwa furaha aliyokuwa nayo hakupata hata shida ya  kusoma yaliyomo katika barua hiyo, na aliamua  kuacha na kuelekea jikoni kumpikia mumewe chakula cha jioni ambacho muwewe huwa anakipenda kula 🌃 hasa nyakati za usiku.

Baada ya kupika na kuweka mezani, alienda kwenye chumba cha na kuoga,na alipomaliza alitoka  kisha akavaa gauni lake la kuvutia zaidi la usiku,( night dress👗) kisha akajitupia kitandani.

Wakati alipojitupia kitandani, ghafla mumewe akabisha hodi, 

Na aliposikia alienda na kumkaribisha ndani,

Kwa furaha alizokuwa nazo, alifika na kufungua mlango ile tu mumewe alipomwona  alikasirika sana.

Mkewe alishangazwa na hali aliyokuwa nayo mumewe na akauliza  bby lakini  kwa nini hujaniruhusu nikukumbatie, lakini mumewe hakujibu kitu, alizidi kumkazia sura iliyojaa hasira,.

Mume akauliza, "Je! Umesoma barua ambayo nimekuachia mezani?"

Mwanamke akajibu, "Ah... ndio nimeona.

Ndio maana nimeamua kukuandalia chakula ukipendacho my.

Asante sana mume wangu barua , ilikuwa tamuuu.. sana "

Akamwinamia  ili ampe busu lakini mumewe  alimsukuma na mke alibaki  kushangaa.

Mume akaendelea, "Ikiwa ulisoma , basi kwa nini haujafanya chochote ambacho nilikuamuru ufanye"?

Mume wake aliingia ndani na akatoka haraka huku kabeba begi lake la nguo.

Akaelekea moja kwa moja mpaka  mlangoni  na akamwambia mkewe, 

"Tutaonana baada ya siku 7."

Mwanamke alisimama akiwa amechanganyikiwa lakini kabla ya kusema neno, mlango ulifugwa 

Alirudi kwenye meza ya kula ili kuangalia barua hiyo ilikuwa inasema je,

Ilisomeka hivi ……

Mke wangu mrembo, Kampuni yangu imeniteua mimi na  wenzangu 4  tuende safari ya siku saba huko Dubai kwenye programu ya mafunzo.

Walisema kwamba tunaweza kwenda pamoja na wake  zetu na nilidhani hii itakuwa fursa nzuri kwa sisi kuwa na ( kishilio) honeymoon ambayo  hatukuwahi kufanya baada ya kufunga ndoa yetu, 

Tayari nimeandaa nguo zangu mwenyewe bby usipate shida mke wangu , kwa hivyo tafadhali jiandae na wewe.

Ndege yetu inaondoka saa moja kamili jioni kwa hivyo nitakuwa nyumbani saa kumi na mbili tayari  kwa sisi kwenda uwanja wa ndege.

Hakuna haja ya kupika chakula cha jioni kwani kutakuwa na chakula kwenye ndege.

Jitayarishe nitakaporudi, nikutoka tu . 

Tafadhali kuwa tayari kabla sijarudi ili tusikose ndege.

Ninakupenda kwa dhati.

Unadhani mwanamke huyu hakuwa na busara wakati unasoma kipande hichi utagundua, jambo,

Kwa bahati mbaya hii ni hali ya Wakristo wengi katika Mwili wa Kristo leo.

Tumemkubali Yesu kama Bwana wetu, na tunafurahi kuwa watoto wa Mungu na ukweli ni kwamba atarudi tena kwa ajili yetu siku moja.

Lakini hatujazingatia kile Yeye anatarajia tufanye kabla ya kurudi kwake.

Hii ni kwa sababu Bibilia zetu zimefungwa.

Tunasoma maandiko machache katika bibilia na tunafurahi juu ya ahadi zake lakini tumepuuza kabisa maagizo yake.

Humjui mwanaume  ikiwa hujui Neno lake.

Je! Ni vipi basi tunadai kuwa tumeolewa na bwana harusi ambaye neno lake tumelitoa nyuma katika harakati za kutafuta ishara na maajabu.

Kwa bahati mmbaya ambayo wengi hawajui ni kwamba Neno ndilo  nguvu ya ishara na maajabu, kwa hivyo ikiwa tutakwenda kwa neno hili vitu ambavyo tunafuatilia vitatufuata.

Wacha tuangalie barua yake, ambayo ni Neno la Mungu.

Itatuvuta karibu na utashi wake kwetu na kutuwezesha kutembea katika ushindi juu ya ulimwengu huu na changamoto zake,.

TAFADHALI SAMBAZA BARUA HII KWENYE VIKUNDI KADHAA, IKIWA UNAHISI YAPASWA KUSOMWA NA JAMII YAKO,.

No comments