jinsi ya kuwashinda maadui zako(hatua 3 muhimu)
JINSI YA KUWASHINDA MAADUI ZAKO
(Hatua tatu muhimu)
______________________________________________________________________
Katika maisha hakuna asiye na adui. Kwa kadiri unavyoongeza marafiki na maadui zako ndivyo wanavyozidi kuongezeka katika maisha yako, lakini hiyo isikuzuie kuishi karibu na maadui zako kwani maadui wanafaida pia ikiwa utaishi nao kwa akiri. Tunaweza kuishi nao bila kuwaogopa na kuwashinda kwa urahisi kwa kufanya yafuatayo:
1. Tambua aina ya maadui ulionao, hii ni kwa sababu si maadui wote wameumbwa kwa kufanana, maadui wana uwezo tofauti kutegemea uhusiano ulinao nao na asili yao. Pia unahitaji kujifunza zaidi jinsi wanavyofanya kazi za uadui kwako.
2. Waweke karibu na wewe, usiwe mtu wa kuwakimbia adui hii itakusaidia kujifunza zaidi jinsi walivyo. Kama unavyowaweka karibu marafiki zako , na maadui zako waweke karibu pia ili upate njia za kuwashinda .
3. Tafuta udhaifu wa maadui zako, kila adui ana udhaifu wake. Haijalishi zako wanaonekana imara kwa kiasi gani. Kujua udhaifu wa maadui zako itakusaidia kuandaa na kupata mbinu za kuwashinda.
ENDELEA KUPAMBANA ..............!!!!!!
Post a Comment