umuhimu wa Malaika/kazi zake ktk maisha yetu!

Kila atakayekombolewa ataelewa huduma ya malaika katika maisha yake binafsi. 
Malaika yule aliyekuwa mlinzi wake tangu maisha yake ya awali kabisa; malaika yule aliyechunga hatua zake na kufunika kichwa chake katika siku ya hatari; malaika yule aliyekuwa naye pale kwenye bonde la uvuli wa mauti, yule aliyeonesha mahali pake pa pumziko, yule aliyekuwa wa kwanza kumsalimu katika asubuhi ile ya ufufuo - itakuwaje kuzungumza pamoja naye na kujifunza historia ya kuingilia kati kwa Mungu katika maisha ya mtu binafsi, na ya ushirikiano wa kimbingu katika kila kazi ya wanadamu! 

Mifadhaiko yote ya uzoefu wa maisha wakati huo itawekwa wazi. Pale ambapo kwetu sisi tumeona mchafuko na kukata tamaa, makusudio yaliyovunjika na mipango iliyozuiwa, tutaona kusudi kuu lenye kushinda, linalobatilisha, upatanifu wa kimbingu. 
 
Pale wale wote waliotenda pasipo roho ya ubinafsi wataona matunda ya kazi zao. 

-Joveth Kuboja


Barikiwa

USISAHAU ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv

No comments