amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

Jumanne 28/07/2020

*MUNGU HUTUPATIA YALIYO MEMA*

*Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo.* 
Mhubiri 2:26

📜 Ujana hauwezi kufanywa kuwa makini na wenye taratibu kama uzee, mtoto kuwa mwenye busara kama baba. Wakati ambapo burudani za dhambi zinakatazwa... toa badala yake burudani zisizo mbaya, ambazo hazitatia doa au kupotosha maadili. 

📜 Kuna tofauti kati ya mapumziko na burudani. Mapumziko, ya kweli, huelekea kuimarisha na kujenga. Yakitutoa kutoka katika shughuli na kazi zetu za kawaida, yanatoa kiburudisho kwa akili na mwili, na kwa hivyo yanatuwezesha kurudi tukiwa na nguvu mpya katika kazi ya kweli ya maisha. Burudani, kwa upande mwingine, hutafutwa kwa sababu ya starehe, na mara nyingi huzidishwa kupindukia; inanyonya nguvu zinazohitajika kwa ajili ya kazi yenye manufaa, na kwa hivyo kuwa kizuizi cha mafanikio ya kweli ya maisha. 

📜Wakati tunaepuka yasiyo ya asili na bandia... lazima tuwe na vyanzo vya starehe ambavyo ni safi na vyema na vyenye kuinua. Likizo zetu hazipaswi kutumiwa katika kujifananisha na ulimwengu, lakini hazipaswi kupitishwa bila kutambuliwa.... Katika siku hizi... pata kitu fulani kitakachokuwa badala ya burudani za hatari zaidi. 

📜 Hakuna mapumziko ambayo yanawasaidia wao wenyewe tu ambayo yatakuwa baraka kubwa kwa watoto na vijana kama yale ambayo yanawafanya kuwa msaada kwa wengine. Je isingekuwa vyema kwetu kuadhimisha siku kuu kwa Mungu, wakati ambapo tungeweza kuhuisha katika akili zetu kumbukumbu ya kushughulika kwake na sisi? 

🔘 *Ulimwengu una siku kuu nyingi, na wanaume hushughulishwa sana na michezo, na mbio za farasi, na kamari, kuvuta sigara, na ulevi. Wanaonesha wazi ni chini ya bendera gani wanasimama.... Je! watu wa Mungu hawataweza mara nyingi zaidi kufanya mikutano mitakatifu ambayo katika hiyo watamshukuru Mungu kwa baraka zake tele?*

*TAFAKARI NJEMA SANA*

Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv

No comments