Tafuta Amani na watu wote!

Huruma Mungu anayoidhihirisha kwetu, anatutaka nasi tuidhihirishe kwa wengine. 
Hebu wenye harara, kujitosheleza, wenye kisasi, wamtazame Yeye aliye mpole na mnyenyekevu, aliyeongozwa kama kondoo bubu kwa wakata manyoya. 
Na wamuangalie yeye ambaye dhambi zetu zilimchoma na huzuni zetu alizibeba, nao watajifunza kuvumilia, kustahimiliana na kusamehe. 
Kwa njia ya imani katika Kristo, upungufu wote wa tabia utajazwa, uchafu wote utasafishwa, kila kosa litasahihishwa, ubora wote utaongezwa. 

"Na ninyi mmetimilika katika yeye......" Kol. 2:10.

No comments