amka na Bwana
*KESHA LA ASUBUHI.*
Jumapili 19 Julai 2020.
*ILI KUWA NA MARAFIKI INABIDI TUWE WEMA.*
*_Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakiniyuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu. Mithali 18:24._*
✍️Katika mipango kwa ajili ya elimu ya wateule inadhihirishwa kwamba maisha yanayomzingatia Mungu ni maisha ya ukamilifu. Kila hitaji analoliweka moyoni, Yeye anaandaa jinsi ya kulikidhi; kila uwezo aliouweka, anajitahidi kuukuza.
✍️Mwanzilishi wa uzuri wote, Yeye mwenyewe ni mpenda uzuri, Mungu aliandaa ndani ya watoto wake kufurahishwa na upendo wa uzuri. Aliandaa pia kwa ajili ya mahitaji yao ya kijamii, kwa ajili ya ushirika wa wema na wenye kusaidia ambao unatenda mengi sana kukuza huruma na kuchangamsha na kufanya maisha kuwa matamu.
✍️Urafiki wa Kikristo kwa ujumla unakuzwa kidogo sana na watu wa Mungu... Kwa ushirikiano wa kijamii mazoea yanaundwa na mapatano ya urafiki yanafanywa ambayo husababisha umoja wa moyo na mazingira ya upendo ambayo yanapendeza machoni pa mbingu.
✍️Kila mtu atapata marafiki au kujenga urafiki. Na kwa uwiano wa nguvu ya urafiki, itakuwa kiasi cha mvuto ambao marafiki wataweka juu ya kila mmoja wao kwa ajili ya wema au ubaya. Wote watakuwa na washirika, nao watashawishi na kushawishiwa. Kiungo hiki ambacho kinaunganisha mioyo ya wanadamu pamoja, ili kwamba hisi, ladha, na kanuni za watu wawili zipate kuchanganywa kwa karibu sana ni cha ajabu. Mmoja anatambua roho ya mwingine na kunakili njia na matendo ya mwingine.
✍️Kama vile nta inavyohifadhi sura ya muhuri, ndivyo akili inavyohifadhi fikira zinazozalishwa na maingiliano na ushirika. Mvuto unaweza usitambuliwe, lakini si kwamba una nguvu kidogo.... Ikiwa uchaguzi utafanywa kuhusu marafiki wanaomcha Bwana, ushawishi utaongoza katika ukweli, wajibu, na utakatifu. Maisha ya kweli ya Kikristo ni nguvu kwa Mungu.
✍️Vuguvugu la urafiki wa kweli ni mwonjo wa awali wa furaha za mbinguni.
*MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI NENO LAKE.*
🙏🙏🙏🙏
Post a Comment