Kosa
Huwa unafanya nini unapofanya KOSA ambalo linakupa HATIA MOYONI?
Kosa ambalo kila unapolikumbuka unajisikia maumivu moyoni na kujiona haufai.
Mara nyingi majuto ya makosa haya ambayo yameshindwa kuondoka katika mioyo yetu huwa ni chanzo kikubwa cha MAAMUZI MABAYA na KUTOKUJITHAMINI.
Natambua pia kuna watu huwa wanapenda sana kutumia makosa ya mtu aliyoyafanya kama njia ya kumtesa kila wakati kwa kumkumbusha.
Umewahi kukutana nao?
Baada ya YUDA kufanya kosa la kumsaliti Yesu, aliamua kwenda KUJINYONGA.
Baada ya Petro kumkana Yesu alilia na kurudi kuvua na baadaye Yesu alipomuuliza kama anampenda alisema
"Nakupenda", akapewa nafasi nyingine.
Wote walikuwa wafalme, ila baada ya Sauli kukosea aliamua kwenda kwa mganga.
Baada ya Daudi kukosea aliamua kutubu kwa Mungu wake na akasamehewa.
Usiruhusu KOSA ulilofanya huko nyuma LIKATISHE NDOTO ZAKO.
Usiruhusu ujione MNYONGE.
BADO UNA NAFASI.
Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya binagoTv!
Barikiwa sana!
Post a Comment