amka na Bwana

*KESHA LA ASUBUHI* 

IJUMAA, JULAI 31, 2020

*SHIRIKIANA NA WALE WANAOMPENDA MUNGU* 

 *Mimi ni mwenzao watu wote wakuchao, Na wale wayatiio mausia yako.* 
Zaburi 119:63

📚 Kati ya mikusanyiko ya wafuasi wa Kristo kwa ajili ya maburudiko ya Kikristo na mikusanyiko ya kidunia kwa ajili ya anasa na burudani, kutakuwepo tofauti dhahiri. Badala ya maombi na kutajwa kwa Kristo na mambo matakatifu, itasikika kutoka katika midomo ya wapendao anasa za kidunia kicheko cha kipumbavu na mazungumzo hafifu. Dhana yao kwa jumla ni kuwa na wakati wa kujifurahisha. Burudani zao zinaanza kwa upumbavu na kuisha katika ubatili. 

📚 Tunataka mikusanyiko yetu ifanyike nasi tutende kwa jinsi ile ambayo, tunaporudi majumbani kwetu tunaweza kuwa na dhamiri isiyo na kosa kwa Mungu na mwanadamu; ufahamu kwamba hatujamjeruhi mtu au kujeruhiwa na mtu kwa njia yoyote miongoni mwa wale ambao tumeungana nao au kuwa na mvuto wowote wenye kudhuru juu yao. 

📚 Sisi ni wa tabaka lile ambalo linaamini kuwa ni fursa kwetu kila siku ya maisha yetu kumtukuza Mungu duniani; kwamba hatupaswi kuishi katika ulimwengu huu kwa ajili tu ya burudani yetu Sisi wenyewe, ili tu kujifurahisha. Tuko hapa kutoa faida kwa binadamu na kuwa baraka kwa Jamii. 

📚 Wale wanaompenda Mungu kwa kweli hawatajenga urafiki na jamii ya wale wasiompenda Yesu. Watagundua kwamba umoja na mazungumzo ya Kikristo ni chakula cha roho, kwamba katika ushirika wa wale wanaompenda Mungu wanapumua katika angahewa ya mbinguni. Wakristo wataonesha upendo na huruma kila mmoja kwa mwenzake. 

🎀 *Kutiana moyo kwa mtu na mwenzake, heshima inayooneshwa na mtu kwa mwenzake, misaada, mafundisho, kukemea, maonyo, ushauri wa Kikristo ambao unapaswa kupatikana miongoni mwa wafuasi wa Kristo utawaendeleza katika maisha ya kiroho; kwa kuwa ushirika wa Kikristo unapatana na mpango wa Mungu.... Watawajali kwa wema wale wote walio na imani ya thamani sana kama wao, nao watavutwa kwenda kwa wale ambao wanampenda Mungu. Kutakuwa na ushirika ambao haujawahi kuwepo ulimwenguni.*

Barikiwa

Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya Binagotv

No comments