amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

Alhamisi 30/07/2020

*USITEMBEE KATIKA NJIA YA WENYE DHAMBI*

*Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali ... Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.* Mithali 1:10-15

💎 Maburudisho yanafanya zaidi kubatilisha utendaji kazi wa Roho Mtakatifu kuliko kitu kingine chochote, na Bwana huhuzunishwa. Wale ambao tabia na uzoefu wao wa kidini ni wa juu juu hufanya haraka sana kukusanyika kwa ajili ya anasa na burudani, na mvuto wao unawavutia wengine. Mara nyingine vijana wa kiume na wa kike ambao wanajaribu kuwa Wakristo wanaofuata Biblia wanashawishiwa kujiunga kwenye karamu hiyo. 

💎 Kwa kuogopa kufikiriwa kuwa ni wa ajabu, na kwa kawaida wenye mwelekeo wa kufuata mfano wa wengine, wanajiweka wenyewe chini ya ushawishi wa wale ambao, huenda, hawajawahi kuhisi mguso wa Mungu katika akili na moyo. Kama kwa maombi wangelijielekeza kwa Matarajio ya Mungu, ili kujifunza yale ambayo Kristo alisema kuhusu matunda yatakayozaliwa juu ya mti wa Kikristo, wangeliweza kugundua kuwa burudani hizi kwa hakika zilikuwa ni tafrija zilizoandaliwa ili kuzuia mioyo kupokea mwaliko wa karamu ya harusi ya Mwanakondoo. 

💎 Wakati mwingine inatokea kwamba kwa kwenda mara kwa mara katika maeneo ya burudani, vijana wale ambao wamekwisha kufundishwa kwa uangalifu katika njia ya Bwana hujisahau na kubebwa na uzuri wa mvuto wa kibinadamu, na kujiambatanisha na wale ambao elimu na mafunzo yao yamekuwa ya tabia ya kidunia. Wanajiingiza katika maisha ya utumwa wa kudumu kwa kuungana na watu ambao hawana mapambo ya roho kama ya Kristo. 

💎 Utaalikwa kuhudhuria katika sehemu za karamu.... Ikiwa wewe ni mkweli kwa Kristo wakati huo, hutajaribu kutoa udhuru wa kutokuhudhuria kwako, bali kwa uwazi na kwa staha utatamka kuwa wewe ni mtoto wa Mungu, na kanuni zako hazikuruhusu kuwa mahali, hata kwa tukio moja, ambapo usingeliweza kukaribisha uwapo wa Bwana wako. 

🔘 *Mungu anatamani kuwa watu wake waoneshe kwa maisha yao manufaa ya Ukristo juu ya anasa za ulimwengu; kuonesha kuwa wanafanya kazi katika kiwango cha juu, kitakatifu.*

*TAFAKARI NJEMA SANA*👮‍♂️

Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv

No comments