Maombi:siku ya 58
🕊 SIKU 100 ZA MAOMBI 🕊
Siku ya 58, Jumamosi, Mei 23, 2020
HERI MASKINI
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao – Mathayo 5:3
“Wale wanaojua kwamba hawawezi kujiokoa wenyewe, au wao wenyewe hawawezi kufanya tendo lo lote la haki., ni wale wanaoukubali msaada anaoweza kutoa Kristo. Hao ndio maskini wa roho, ambao alitamka kuwa wana heri. Anaowasamehe Yesu, huwapa toba kwanza, na ni kazi ya Roho Mtakatifu kuthibitisha dhambi. Wale ambao mioyo yao imeguswa kwa ushawishi wa Roho wa Mungu huona kuwa hakuna cho chote chema ndani yao. Wanaona kwamba yote waliyowahi kufanya ni mchanganyiko wa ubinafsi na dhambi. Kama yule mtoza ushuru maskini wanasimama mbali, hawathubutu kuinua macho yao mbinguni, na wanalia, ‘Mungu unirehemu mwenye dhambi’. . . Wote wenye ufahamu wa kina cha umaskini wa roho zao, wanaojihisi kuwa hawana cho chote chema ndani yao, wanaweza kupata haki na nguvu kwa kumtazama Yesu. – Thoughts from The Mount of Blessing, pp. 7-8
Maswali ya Moyoni:
Kujihesabia haki – mtazamo unaosambaa na mara nyingi bila kujua, unatudanganya ili tufikiri na kujisikia kuwa sisi ni wema – ni kikwazo kubwa sana katika kuupokea kiukweli wokovu binafsi katika Yesu. Tunapotambua umaskini wetu kiroho, hitaji letu la kumpata na kutambua umaskini wetu kiroho, hitaji letu la kumpata la Yesu maisha yetu yote, na kama matokeo yake kumtumainia yeye pekee, wakati hadi wakati, kwamba atatuponya kikamilifu dhidi ya kila dalili ya ubinafsi, ndipo tutakapoweza kuwa na uhakikisho wa wokovu. Kwa nini leo, usije kwa Yesu kama ulivyo, ukiwa na nafsi yako yenye dhambi, iliyovunjika? Kwa nini usidai tu damu yake, maisha yake na mauti yake, kama njia ya wokovu? Kwa nini usimwombe ang’oe hali yote ya kujitegemea iliyo bado moyoni mwako na kuibadilisha na imani katika uweza wake kukuokoa, na kukupatia nguvu kutenda matendo mema yanayosukumwa na upendo usio na ubinafsi?
Taarifa za Sifa:
👉🏽 Nolubabalo D., anasema “Asante Bwana kwa mkono wako kwa ajili ya Afrika. Asante kwa ulinzi wako. Asante kwa kuwatunza watoto wangu ninapokuwa sipo. Unastahili sifa zote.”
👉🏽 Philippe M., anasema “Katika mji wetu wa Kananga, hakukuwa na matangazo ya redio kabla ya mazuio ya Covid-19, lakini wakati huu wa zahama tunarusha matangazo manne kila juma kupitia vituo vinne vya redio mahalia. Tunamshukuru Mungu kwa hilo!”
MAMBO YA KUOMBEA
1️⃣ Omba Yesu akutakase dhidi hali yote ya kujihesabia haki na akupatie utambuzi wa
hitaji lako kubwa la kila siku na la maisha yote la kumhitaji yeye.
2️⃣ Ombea wainjilisti kule Afrika ya Kusini wanaopambana na masuala mbali mbali ya
kiafya na msongo. Ombea ili waponywe na kuwezeshwa kupata njia za kuhubiri injili
hata sasa.
3️⃣ Mwombee Kaka Samuel S. anasumbuliwa na maumivu makali sehemu ya chini ya
mwili wake na madaktari hawajui tatizo ni nini. Pia mwombee dada Tabitha N. aliyepimwa na kugundulika kuwa anatundu katika moyo wake na yupo kwenye maumivu makali. Ombea wapone na pia uponyaji wa wengine wengi wanaoteseka muda huu.
4️⃣ Ombea Kituo cha Huduma ya Wachina kule Jakarta, Indonesia wanapoendelea kuendesha mikutano ya injili kwa njia ya mtandao kila Sabato tangu Mei 9 hadi Juni 20, 2020. Mkutano wa kwanza ulivuta zaidi ya watazamaji 3000 na zaidi ya 260 kati yao walijiandikisha kwenye masomo ya Biblia.
MUNGU AWABARIKI

Post a Comment