Maombi:siku ya 55

SIKU 100 MAOMBI

*Siku ya 55, Jumatano, Mei 20, 2020*

_*KUJITOA KWA KANISA LAKO MAHALIA*_

Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika – Acts 4:32 

_“Waongofu wa injili walikuwa na ‘moyo mmoja na roho moja.’ Shauku moja iliwaongoza wote – mafanikio ya utume ya waliopewa dhamana; tamaa haikuwa na nafasi maishani mwao. Upendo kwa ndugu na kazi waliyokusudia, ulikuwa mkubwa kuliko upendo wao kwa fedha na mali. Kazi zao zilishuhudia kwamba walizihesabu roho za watu kuwa ni za thamani kubwa kuliko utajiri wa kidunia. Ndivyo itakavyokuwa daima Roho wa Mungu anapoyamiliki maisha.” – Acts of the Apostles, 70_

 *Maswali ya Moyoni:*

```Kuna nyakati ambapo huwa tunaweza kuchanganyikiwa na kanisa letu mahalia au hata kanisa la ulimwengu. Lakini bado tunajua kuwa kanisa ni mchumba wa Kristo. Ikiwa Yesu amejitoa hivyo kwa kanisa, si inatupasa sisi tujitoe kwake pia? Wakristo wa awali walijazwa na Roho na walikuwa tayari kutoa kafara yote kwa ajili ya kanisa na utume. Kwa nini leo usimwombe Mungu akusamehe kwa ajili ya baadhi ya mitazamo ya dhambi unayoweza kuwa nayo dhidi ya mchumba wake, na kumwomba akubatize kwa ubatizo wa Roho wake, akikupa nguvu za kuutafuta umoja, na kuishi maisha ya kujitoa kafara ili kusaidia na kubariki jumuiya ya kanisa lako mahalia.```

*Taarifa za Sifa:*

• Tunamsifu Mungu kwa ajili ya makanisa mapya 900 yaliyoanzishwa katika miaka michache iliyopita katika Divisheni ya Kusini mwa Amerika.

 • Katika Divisheni ya Kusini mwa Amerika mahitaji ya watu kujifunza Biblia yameongezeka mara 5 zaidi tangu zahama hii ilipoanza!   

MAMBO YA KUOMBEA

 • Ombea kanisa katika nchi ya Gabon. Ombea washiriki wake wawe na moyo na hekima ya kuwafikia raia wenzao. Kwa namna ya pekee ombea kundi la Akanda ambao wanajaribu kuwahudumia wale wenye ulemavu.

 • Ombea mahitaji ya kanisa lako mahalia. Ombea umoja, uponyaji na kujitoa upya kwa ajili ya kushuhudia na shughuli za utume.

• Ombea wachungaji na viongozi wa kanisa katika baadhi ya maeneo ya Unioni ya Haitia. Ombea kanisa katika baadhi ya maeneo ya Haiti ambayo yamejaa vikundi vya majambazi wenye silaha. Ombea afya ya kiroho, kimwili, kifedha na kiakili ya washiriki wa Haiti.

 • Ombea washiriki walioyapokea mafundisho potofu au mtazamo uliogeuzwa na wanajaribu kuwadanganya wengine.

• Ombea washiriki wa zamani waliojitenga na kanisa na kuunda makundi yao au madhehebu yao. Waombee ili waongozwe kwenye ukweli.

No comments