Amka na Bwana
KESHA LA ASUBUHI
Jumatano 20/05/2020
*KIASI KATIKA MASOMO*
*Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wowote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili.* Mhubiri 12:12.
📝 Jitihada za akili pasipo mazoezi ya mwili ya kutosha husababisha usiwepo uwiano mzuri wa mzunguko wa damu ubongoni. Ubongo unakuwa na damu tele ila sehemu za pembezoni zinakuwa na uhaba mkubwa wa damu. Muda wa kusoma na muda wa michezo sharti uwianishwe vizuri, na muda upatikane wa kutenda kazi za mikono...
📝 Afya haiwezi kuwa njema hadi pale muda unapotengwa kila siku kwa ajili ya mazoezi kwenye hewa safi nje. Muda maalumu utengwe kwa ajili ya kazi fulani za mikono, jambo litakalofanya viungo vyote vya mwili viingie kazini. Shughulika na kazi za kiakili huku ukijipatia muda wa mazoezi ya mwili, ili akili iweze kupata burudiko.
📝 Ubongo wa watu wenye kufanya kazi za kufikiri hutenda kazi ngumu sana. Hutesa nguvu zao za kiakili wakijiaminisha kuwa lipo kundi jingine la watu ambao ni jukumu lao kushughulikia kazi ngumu za mikono. Kundi hilo ubongo wao hauteswi, ila misuli yao ndiyo hutumika kikamilifu. Ubongo wao hupokonywa nguvu za kuwaza; kama vile ubongo wa wenye kufikiri unavyoteswa mno, wakati miili yao inavyopokonywa mazoezi ya misuli. Afya nzuri yabidi ishirikishe mazoezi ya mwili na ubunifu wa kiakili.
🔘 *Nyanja zote za kimaadili, kiakili, na kimwili sharti ziwe na uwiano mlinganifu ili kuwa na wanaume na wanawake wenye afya njema. Baadhi wana taaluma zinazowaruhusu kutumia sana akili zao, wakati wengine furaha na mwelekeo wao upo kwenye kazi za mikono. Matabaka yote haya yapaswa kuboresha kule walikopungua, ili waweze kuitoa miili yao "iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana " (Warumi 12:1). Afya yapasa kutunzwa vyema kama tabia*
*TAFAKARI NJEMA SANA*👮♂️

Post a Comment