Maombi:siku ya 54
*SIKU 100 ZA MAOMBI.*
Siku ya 54, Jumanne, Mei 19, 2020.
KUJITOA KWA MWENZI /FAMILIA YAKO.
Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Enyi waume, wapendeni wake zenu,
kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; Enyi watoto, watiini wazazi
wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana. – Waefeso 5:22, 25; 6:1, 4.
Kinachosababisha mgawanyiko na ugomvi katika familia na ndani ya kanisa ni kujitenga na
Kristo. Kumkaribia Kristo ni kukaribiana kila mmoja na mwenzake. Siri ya umoja wa kweli
ndani ya kanisa na katika familia sio diplomasia, sio usimamizi, sio juhudi za mtu asiye wa
kawaida za kushinda magumu – ingawa mengi ya hayo yatahitajika – lakini ni mwunganiko na
Kristo.” do—but union with Christ.” – The Adventist Home, 179.
*Maswali ya Moyoni:* Mwenzi wako na familia yako ni watu ambao maishani mwako unao
wajibu makini; Kuwapenda, kuwasaidia, na kuwafundisha katika uhusiano wa furaha na upendo
pamoja na Yesu. Je! Leo utajitoa ili kuwapatia rehema, msamaha, na upendo sawa na aliotoa
Yesu kwako, kwa mwenzi wako na kwa familia yako? Je! Ni shauku yako kuwa kiongozi wa
kiroho kwa ajili ya nyumba ayako? Mwombe Yesu leo aweze kutembea na wewe kwa kina na
mwunganiko pamoja naye ili uweze kumuakisi vema kwa mwenzi na kwa familia yako.
Taarifa za Sifa:
1. Prosper, O., anasema, “Ndiyo! Haijalishi kuna COVID-19, nitadumu kuimba sifa kwa
Bwana Aliye Juu.”
2. Jon, W., anasema, “Zahama hii imenipatia shauku mpya ya kutembea na Kristo kwa
karibu zaidi!”
*MAMBO YA KUOMBEA:"
1. Mwombee mwenzi wako, wazazi, watoto, ndugu zako, na wanafamilia wengine.
Waombee ili wamjue Bwana Yesu Kristo. Omba ili uwe mwenzi, mzazi, ndugu,
mwana/binti kama anavyotaka Yesu uwe.
2. Ombea Siku ya Maombi ya Ndoa & Familia (Juni 6, 2020) iliyoandaliwa na Idara
Huduma za Familia ya Konferensi Kuu. (Tembelea: family.adventist.org) .
3. Ombea watu wanaoishi peke yao wakijisikia upweke sana hasa wakati huu. Waombee
ili waone mibaraka ya kuwa peke yao hasa katika kumtumikia Mungu. Omba kwamba
kama ni mapenzi ya Mungu waweze kupata wenzi wacha Mungu.
4. Ombea watu wanaopambana na uraibu.
5. Ombea mshiriki wa kanisa kule Trinidad ambaye binti yake aliuawa miaka miwili
iliyopita, na kijana wake wa kiume aliuawa mwezi Machi mwaka huu. Mwombee ili apate faraja na pia apate ulinzi kwa familia yake iliyosalia.
*MUNGU TUSAIDIE ILI TUJITOE KWA WENZI WETU NA FAMILIA ZETU KIKAMILIFU, KAMA WEWE ULIVYOJITOA KWETU SOTE UKATUOKOA.*
🙏🙏🙏🙏

Post a Comment