Amka Na Bwana!
KESHA LA ASUBUHI
Jumanne 19/05/2020
*USIGEUZE MCHANA KUWA USIKU*
*Ewe mvivu,utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?*
☄️ Afya ni hazina ya thamani kuu. Ndiyo hazina bora wanadamu wawezayo kumiliki. Utajiri, heshima au elimu vitowekapo vyaweza kurejeshwa kwa gharama fulani; ila siyo Afya. Huwezi kuwa na furaha endapo unapewa vitu vyote hivyo ila ukose afya. Ni dhambi kubwa ya kutisha kuchezea afya ambayo Mungu amekupatia, kwani kila mzaha dhidi ya afya huleta madhara ya kudumu, iwe hasara kuu kwetu, na hatimaye kupoteza uhai.
☄️ Ni tabia iliyozoeleka jinsi gani kuubadili mchana kuwa usiku, na kuubadili usiku kuwa mchana. Vijana wengi hulala usingizi asubuhi, ambapo walipaswa kudamka mapema wasikiapo ndege wa angani wakiimba. Hebu vijana wawe na kawaida ya kutunza muda wa kwenda kulala na muda wa kuamka. Hebu wanuie kwa dhati kuwa watajiweka wenyewe chini ya nidhamu; wakienenda kulingana na kanuni. Mungu ni Mungu wa utaratibu, na ni jukumu la vijana kuzingatia kanuni, kwani kwa kufanya hivyo ni kwa faida yao nafsini.
☄️ Maadamu kazi ya ujengaji mpya mwili hutendeka wakati mtu amelala, ni muhimu, hasa kwa vijana, muda wao wa kulala uwe rasmi tena wa kutosha. Wengi wa vijana wapenda anasa huudhuria starehe za usiku na kutumia saa zile ambazo Mungu amewapatia ili wapumzike na kulala ili kuurejeshea mwili afya. Wanayapokonya mashavu tabasamu ya afya, na uzembe huo huujaza kwa kutumia vipodozi.
🔘 *Je si ingekuwa busara kuachana na tabia hii ya kugeuza usiku kuwa mchana; na saa za asubuhi kuwa usiku? Iwapo vijana watajenga mazoea ya kuwa na mpangilio na utaratibu, watafanikiwa kiafya, kiroho, kiakili na kiahiba.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮♂️

Post a Comment