Maombi:siku ya 53
🕊MAOMBI YA SIKU 100🕊
Siku ya 53, Jumatatu, Mei 18, 2020
KUJITOA KWA AJILI YA MARAFIKI
Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu. - Mithali 18:24
“Yonathani, kwa kuzaliwa alikuwa mrithi wa ufalme, lakini alijua kuwa amewekwa kando kwa amri ya Mungu; kwa ajili ya mpinzani wake rafiki mpole na mwaminifu kuliko wote, aliyakinga maisha ya Daudi kwa uangamivu wake mwenyewe;... jina la Yonathani linathaminiwa mbinguni, na linasimama duniani kama shahidi wa uwepo na nguvu wa upendo usio na ubinafsi. – Education, 157
Maswali ya Moyoni:
Urafiki wa Yonathani na Daudi ulikuwa na ubora wa kiroho na kina ambacho hakionekani hata kwa uchache. Msingi wa urafiki wao ulikuwa ni agano takatifu la kusaidiana kiroho baina yao na kujitoa. Je! Unao marafiki wa kiroho? Je! Wewe ni rafiki wa kiroho wa mtu fulani? Kwa nini usichague kujitoa kwa ajili ya maendeleo ya kiroho ya rafiki zako kwa kuweka kando tamaa na raha zako binafsi, na kutoa muda na upendo wako kuwasaidia rafiki zako katika kutembea kwao na Kristo?
Taarifa za Sifa:
👉🏽 Mikutano ya injili inayoendeshwa na huduma ya It is Written kwa njia ya mtandao inaleta matokeo ya kushangaza ambapo maelfu ya watu wanahudhuria na wengi wanafanya uamuzi kumpokea Yesu. Watafutaji ukweli wanajiunga na makanisa mahalia ya Kiadventista kwa ajili ya ufuatiliaji.
👉🏽 Watu wengi ambao zamani walikuwa washiriki wa Kanisa la Waadventista wanajiunga na kanisa, asante kwa ongezeko la shughuli za ushuhudiaji kwa njia ya mtandao.
MAMBO YA KUOMBEA
1️⃣ Omba kwa ajili ya marafiki zako, na hasa wale wasiomjua Kristo au waliopotea katika njia zao. Omba kwamba Mungu akupatie moyo wa kuwa na mvuto wa kiroho ulio chanya na makini katika maisha yao.
2️⃣ Omba kwa ajili ya mikutano ya injili iliyopangwa kufanyika kule Rift Valley, Kenya, eneo ambalo halijaingiwa na kanisa letu.
3️⃣ Omba kwa ajili ya kituo cha huduma za jamii cha Kanisa la Waadventista wa Sabato liitwalo Phoenix Beacon Light wakati washiriki wapya wakikiandaa ili kianze kuhudumia jamii yao.
*MUNGU AWABARIKI*

Post a Comment