Amka na Bwana!


KESHA LA ASUBUHI

Jumatatu 18/05/2020

*KIASI KATIKA KAZI*

*Tazama, mimi niliyoyaona kuwa ndiyo mema na ya kufaa, ni mtu kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote anayoifanya chini ya jua, siku zote za maisha yake alizopewa na Mungu, maana hilo ndilo fungu lake.* Mhubiri 5:18

🔷 Muda huo utakuwa umetumika kwa busara endapo umeelekezwa katika kuimarisha na kuhifadhi afya ya kimwili na kiakili. Ni jambo rahisi kupoteza afya, ila ni jambo gumu sana kuirejeza upya afya. Tuwe na tahadhari tusiumize au kudhoofisha kazi mojawapo ya utendaji wa mwili au akili kupitia kufanya kazi kupita kiasi au kutumia vibaya sehemu yoyote ile ya mwili.

🔷 Wale ambao huweka juhudi zao kukamilisha kazi fulani kwa muda fulani uliopangwa, kisha wakaazimu kuendelea na kazi wakati mwili wao umechoka wataka pumziko, hawana la kufaidi. Wanaishi kwa mtaji wa nguvu za mkopo. Wanatumia nguvu za uhai ambazo watazihitaji siku za usoni.  Na uzee uwafikapo ambapo nguvu hizo zitahitajika sana, watakuwa hawanazo maana wameishazitumia kizembe leo. Kila mmoja anayekiuka sheria za afya ajue hakika kuwa huko mbeleni atateseka kwa namna moja au nyingine.

🔷 Uchovu na uchakavu unaowakabili wengi wetu leo siyo mzigo Mungu aliowatwisha; ila wao wenyewe wamejisababishia matatizo ya kiafya kwa vile wameamua kutenda mambo yale ambayo neno la Mungu liliwakataza kufanya. Kamwe hatupaswi kujiweka kwenye mazingira ambapo tutafanya kazi kupita kiasi. Baadhi, kwa nyakati maalumu, waweza kulazimika kutenda kazi kupita kiasi, hiyo yapasa iwe kwa nadra wakati wa dharula, na kamwe isiwe ndiyo kanuni ya utendaji.

🔘 *Iwapo tutamheshimu Mungu kwa kutenda sehemu yetu, kwa upande wake atatenda kuhifadhi afya zetu. Kwa kuwa na kiasi katika kula, kiasi katika kunywa, kiasi katika uvaaji, kiasi katika kazi, kiasi katika mambo yote, twaweza kujihakikishia afya bora asiyoweza kutoa daktari awaye yote. Usilundike kazi za siku mbili ndani ya siku moja.*


*TAFAKARI NJEMA SANA*👮🏽

No comments