Amka na Bwana!
KESHA LA ASUBUHI
Jumanne 26/05/2020
*AMANI KATIKA DHAMIRI SAFI*
*Wana amani nyingi waipendao sheria yako, wala hawana la kuwakwaza.* Zaburi 119:165.
🔷 Iwapo akili iko huru na yenye furaha, ikijisikia amani na kuridhika kwa sababu ya mema iwatendeayo wengine, huunda tabasamu itayoleta badiliko chanya kwenye mfumo mzima wa mwili, ukisababisha damu izunguke vizuri mwilini na mwili utende kazi kwa ufanisi.
🔷 Baraka za Mungu ni nguvu ya uumbaji, na wale wanaojali kuwahudumia wengine watatambua baraka hizo za ajabu moyoni na maishani mwao. Wale ambao hufuata njia ya hekima na utakatifu hawatajilaumu kwa muda uliotumika kuhudumia wengine, wala hawatasumbuliwa na huzuni au fadhaa ya akili kama ilivyo kwa wengine, isipokuwa kama hujishughulisha na anasa na starehe zisizofaa.
🔷 Starehe zaweza kuuchangamsha ubongo, ila fadhaa hakika itafuata. Kazi yenye tija pamoja na mazoezi ya viungo vya mwili vitakuwa na mvuto wa kiafya ubongoni, kuimarisha misuli, kufanikisha mzunguko wa damu, na kuwa wakala bora katika urejeshaji wa afya...
🔷 Kutambua kuwa unatenda haki ni dawa nzuri kwa akili na miili iliyodhaifu. Mibaraka maalum ya Mungu kwa mtu huyo ni afya na nguvu. Kutenda mema ni kazi ambayo humnufaisha mtoaji na mpokeaji. Iwapo unaacha ubinafsi ili kuwajali wengine, unapata uponyaji wa maradhi yao.
🔘 *Furaha utakayokuwa nayo sababu ya kutenda mema itakusaidia sana katika kukuza mawazo yaletayo tiba. Furaha ya kutenda mema huchangamsha akili na furaha hiyo husambaa mwili mzima. Mtu ambaye akili yake ni tulivu ametulia miguuni mwa BWANA yupo katika njia sahihi ya afya.*
*TAFAKARI NJEMA SANA*👮♂️
Post a Comment