RODRI ni mido kisheti


 Ukiliacha suala la Manchester City kutolewa UEFA Champions League , basi Rodri ndie mchezaji anayenivutia zaidi kwenye kikosi cha Pep kwanini?


1: Mechi baada ya mchezaji anakupa performance bora sana , sio mchezaji ambaye atachagua mechi za kukiwasha bali ni mchezaji ambaye kila mechi anakupa vitu vinavyohitajika ( consistency ) hapa ndio utapata kuona ni "mchezaji bora" na sio "mchezaji okay"


2: Uwezo wake wa kucover eneo kubwa la uwanja kwa uzuri , ni wa hali ya juu sana yaani kuna wakati anacheza kama kete 8 kiwanjani lakini kumbe ni kiungo wa ulinzi haswa , "offensive" kuna wakati mabeki wa pembeni hupanda juu sana hufanya cover kwenye maeneo hayo


3: Kutoka kwenye pressure akiwekewa na mpinzani ( pressure resistance ) mchezaji ambaye akiwekewa presha kwenye maeneo yote matatu nyuma yake kulia , nyuma yake kushoto , nyuma yake anaweza kutoka kwenye presha na kushinda mipambano



Mchezaji ambaye anaweza kufit kwenye mifumo / miundo tofauti , lakini anajua nini anachokifanya kwenye zone yake ni kumzuia mpinzani , oooh aiseee Rodri ni katili sana pale kati , hii ni siraha adhimu ya Pep akihitaji kushinda mipambano yake kwa wapinzani .!


CC Moshi JR

No comments