"Jumapili ni siku ya kumwabudu shetani"alisema Pasta Lai
Mchungaji wa kanisa la Jesus Celebration Centre (JCC) Mombasa amezua sintofahamu baada ya kudai kwamba siku ya Jumapili sio siku iliyoidhinishwa na Mungu kama sabato bali na shetani ili watu wamwabudu.
Kwenye video iliyosambaa kwa kasi mitandaoni na ambayo itawasisimua wafuasi wa kanisa la Seventh Day Adventist (SDA), Lai aliwashambulia waumini wake kwa kupenda kushiriki sabato Jumapili akisisitiza kwamba matendo yao hayo sio tu ya kishetani bali pia yalidhihaki injili.
Licha ya Lai kuwa mkristo anayeshiriki ibaada siku ya Jumapili, alishikilia kwamba ni makosa kuabudu siku hiyo kwani hiyo ni njama ambayo muovu shetani anatumia ili kuliangamiza kanisa.
Kulingana na mtumishi huyo, Biblia inatambua Jumamosi kama siku ya sabato ambapo kila muumini anafaa kuabudu na wala sio Jumapili kama ilivyo ada kwa Wakristo wengi duniani.
Hata hivyo, itakumbukwa kwamba kanisa lake la Mombasa hufanya ibaada siku ya Jumapili na wala sio Jumamosi jinsi anavyoshauri.
Lai alishikilia msimamo huo pasi na kujali kwamba baadhi ya waumini wa kanisa hilo wangekerwa na ujumbe wake.
"Mungu alisema mkumbuke Sabato na muifanye takatifu. Sabato sio Jumapili. Kama hupendi ujumbe huu, basi hupendi ukweli," alidokeza huku waumini wakisalia kumkodolea macho wasiwe na la kusema
Chanzo:- Tuko

We kama mkristo unaesali Jumapili ,embu toa maoni yako
ReplyDeleteHamna kitu huyo mzee
ReplyDeleteKiaje kaka
Delete