Madrid lazima icheze Fainali ⚽️
Wachezaji huwa wanakuwa sifa zao au niziite ( strength zao ) na wanatofautiana sana , nimependa zaidi alichokifanya Jude Bellingham dhidi ya Man City
1: Alikuwa anacheza kama attacking fullbacks , kwa maana alionekana kwenye build up zote mbili muhimu za Madrid ikiwa inashambulia na kuzuia , pale timu inapokuwa off the ball hataki kuwa abiria ( anajituma sana ) kusaidiana na wenzake kudefend
2: Alikuwa anazuia vizuri njia za mpira ambazo City walikuwa compact sana kulisogelea goli la Madrid , licha ya timu kuwa off the ball mara nyingi lakini aliweza kurudi nyuma kuzuia mashambulizi , pia rotations yake na Valverde ilikuwa nzuri sana kwenye build up kwa kufika kwenye matukio kwa wakati sahihi
3: Alikuwa na utunzaji wa mpira ( ball possession ) nzuri sana , nafikiri ndio mchezaji aliyechezewa faulo nyingi zaidi na City kwasababu akipokea pass kutoka kwa wenzake anaweza kuuficha mpira hata akiwekewa presha kwenye mpira ( pressure resistance )
Binafsi ukiachana na Lunin kuwa bora zaidi kwenye penalties , nafikiri Man Of The Match ni Jude Bellingham kwa performance yake dakika 90 lakini ikiwa Lunin ni okay au Valverde ni sawa : Madrid wale nusu fainali .!
Post a Comment