🚨 Miquissone bado ninamuitaji: Kocha wa Simba
Klabu ya Simba ilipanga kumtoa kwa mkopo kiungo wao mshambuliaji raia wa Mozambique, Luis Miquissone kuelekea msimu ujao ili akarudishe ubora wake kwa kupata muda wa kucheza zaidi.
- Lakini Kocha Abdelhak Benchikha bado anamuhitaji mchezaji huyo kuelekea msimu ujao wa michuano na ameuambia Uongozi wa klabu ya Simba kuwa Luis Miquissone anapaswa kubaki ili aingie nae pre season, Luis Miquissone bado ana mkataba na Simba wa mwaka mmoja.
- Uongozi wa Simba umepanga kufanya kazi na marekebisho mbalimbali katika timu kwa mapendekezo zaidi ya Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha .
Post a Comment