Hizi hapa sababu za Jackson kugombania kupiga Penati
Kwa nini Nicolas Jackson alitaka kupiga penalti dhidi ya Everton:
Jackson alikuwa amefunga bao lake la 10 la Premier League katika kampeni za PL na bao la nne kwa Chelsea Jumatatu, na kumfanya kufika 13 katika mashindano yote.
Inamaanisha kuwa amesawazisha idadi ya mabao ya ligi yaliyofungwa na nyota wa Chelsea, Didier Drogba katika msimu wake wa kwanza akiwa na klabu hiyo - na mabao matatu pekee nyuma ya jumla ya mabao 16 ya nyota huyo wa Ivory Coast katika michuano yote.
Jackson pia alikuwa amejiwekea lengo la kufikia mabao 15 ya Ligi kabla ya kampeni kuisha na alikuwa akitafuta kuongeza penalti hiyo ikizingatiwa kuwa Palmer tayari alikuwa amefunga hattrick.
Cc [Ongea Spoti]
Post a Comment