MAPYA YA IBUKA BAADA YA KIFO CHA MR IBU


 Kufuatia kifo mwigizaji na mchekeshaji wa Nigeria, John Okafor maarufu kama Mr Ibu kilichotokea Machi 2, 2024 mapya yameibuka baada ya kudaiwa kutengwa na wake zake huku binti yake wa kambo akichukua akaunti ya TikTok ya msanii huyo na kubadili umiliki wa akaunti hiyo na kuifanya yake.


Mr Ibu alitalikiana na mke wake wa kwanza ambaye alichukua akiba zake zote huku mke wa pili, Stella Maris akimshutumu kutembea na bintiye wa kambo Jasmine hali iliyopelekea kuugua kisukari. Alipatwa na tatizo la damu kuganda na kufa kwa mishipa ya mguu.


Aliuza mali zake zote na hatimaye mguu wake ulikatwa kutokana na ugonjwa kuathiri mshipa mmoja wa kifundo cha mguu.


 Mkewe wa pili alimtaka amnunulie 'iPhone 15' kwa pesa zilizochangishwa kwa ajili ya matibabu yake wakati akiwa katika hali mbaya. Hata hivyo binti yake wa kambo alifuja pesa hizo za upasuaji sambamba na kujimilikisha akaunti zake za Instagram na TikTok zenye wafuasi zaidi ya milioni moja na kufuta picha zote za msanii huyo.


✍️ Umejifunza nini kuhusu kisa hichi?

No comments