FODEN NI INIESTA MTUPU

FT: Man City 3-1 Man United 

✍🏻Timu bora zaidi imeshinda uwanjani , walitawala kwa maeneo mengi na vitu vingi sana uwanjani , ilikuwa ni suala la muda gani kuliko " kama " Man City watashinda kwa jinsi mechi ilivyokuwa 

✍🏻Man United tangu filimbi ya kwanza uliona nini wanajaribu kufanya 

1: Kuzuia chini zaidi ( lowblock ) kufunga njia za ndani kwenye muundo wa 4-4-2 na kukubali kuacha 1v1 pembeni ya uwanja ( Dalot Vs Doku ) na ( Lindelof Vs Foden ) 

2: Kutumia wingers wao kwa ajili ya counter attacks Rashy na Garnacho huku Bruno na McTominay wakiwa wanashambulia nyuma ya kiungo cha Man City 

3: Kufuata wale Runners pale ambapo City wana mpira , kazi ya Casemiro na Mainoo kuhakikisha KDB na Silva hawatumii sana zile spaces katikati ya Varane na Dalot & Evans na Lindelof 

✍🏻Man City walichokuwa wanafanya ni kujaribu kupasia mpira haraka sana ili kuwa move walinzi na viungo wa United kwa ajili ya kupata space na pia kutumia uwezo wa mawinga wao dhidi ya fullbacks wa United ( Foden pekee alifanikiwa ) kuliko Doku . 

✍🏻Nafikiri baada ya Man City kusawazisha goli ndio pale Man United wakaanza kuchelewa kufika kwenye matukio , wakaanza kusinzia katika nyakati muhimu , wakaacha yote waliyofanya kipindi cha kwanza kwa usahihi hapo ndio Man City hasa Rodri , Stones ambao walikuwa ndani wakaanza kupata space za kutosha kuwalisha ( Foden Silva KDB ) 

Mechi ndio iliishia hapa : 😀

NOTE 

1: Ukiacha goli zuri ambalo amefunga Rashy baada ya hapo unaweka mkono kwenye shavu tu ....🤔🤔

2: Yule Doku kama alituteka tu na ile mechi dhidi ya Bournemouth baada ya hapo daah ... ni kama Antony tu 😀

3: Rodri na Stones wanakupa control , utulivu na uchaguzi sahihi wa pasi zao 

4: Haaland ile ya kwanza alikosaje pale ? Baada ya hapo Amrabat akaona isiwe tabu chukua nyingine hiyo ufunge 

5: Dalot inawezekana kabisa akamaliza msimu kuwa mchezaji bora wa Man United 

6: Spidi ya Walker huwa inawatoa matatizoni wakina Dias pale nyuma , akipatiwa Walker tu basi walinzi wengine kazi wanayo

7: PHIL FODEN ... what a player , muda wote akiwa na mali unaona tu kuna jambo linatokea . 🔥



 


No comments