MAYELE HANA ADABU


 -Kuelewa ni mchakato...kila Mtu amejaaliwa uwezo wake wa kuelewa mambo.


Wengine wanaweza kuambiwa jambo wakaelewa hapo hapo, wengine wanaelewa baada ya dakika 10 na sisi wengine mpaka athari zitokee


Ndivyo tulivyoumbwa...


Mimi awali sikuelewa chochote kuhusu hii picha ila sasa kuna Jambo nimelielewa japo linaweza lisiwe na uhalisia wa asilimia 100.


Ni kwamba...


Kwanza Mayele anaamini MUNGU yupo.


Pili Mayele anaamini MAJINI yapo pia.


Lakini MAYELE huyo huyo haamini katika nyakati alizoziweka MUNGU.


Kivipi...?


Ukimsikiliza MAYELE utagundua kinachomtesa yeye anataka zile nyakati bora alizokuwa nazo akiwa Yanga ziendelee akiwa PYRAMIDS ndio maana kwake KIONGOZI wa YANGA kusema "Sasa hivi Mayele hafungi" limekuwa jambo kuuubwa sana na limemuuma vibaya mno.


Kupitia Imani yake hiyo ya MUNGU Aliamua kujisalimisha ili kuyakwepa MAJINI akiwa nje ya YANGA.


Mimi sijui ukweli kuhusu hayo maneno ya huyo Kiongozi aliyoyasema ila ninachokijua ni kwamba MAYELE wa PYRAMIDS hana namba nzuri kama MAYELE wa Yanga.


Na hili sio viongozi tu wa YANGA hata viongozi wa PYRAMIDS wanajua hilo na ni hali ya kawaida kabisa kwakuwa bado ni mchezaji mgeni anahitaji kuzoea Mazingira etc.


Sasa hizi hasira angezihamishia uwanjani ili huyo KIONGOZI amuone akitupia na kutetema huko kwa waarabu.


Hiki anachokifanya sasa anasahau kuwa mchezaji hana Timu... huwezi kujua kesho anaweza kuwa Chama akarudi kwenye ufalme wake.


Huko aliko Mayele akifeli timu yenye Imani kubwa kwake ni YANGA ambapo aliacha alama.


Ni kama CHAMA tu pale SIMBA...Hajaanzia kucheza Mpira SIMBA lakini Simba imempa mafanikio na kufika hatua ambazo hakuwahi kufika Kabla.


Mwisho Watu wake wa karibu wamkumbushe kuwa kazi yake ni kucheza Mpira na sisi huku nje kazi yetu ni kuongea...akifunga tutamsifia...Asipofunga tutamnanga vile vile, kwani yeye Nani?

No comments