KESI: Rais wa CAF anaipendelea SOUTH AFRICA
Mtandao wa nchini Morocco umeripoti kumtuhumu Rais wa shirikisho la soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe kwa kuhudhuria kila mechi ya Afrika Kusini katika michuano ya AFCON 2023 na hivyo anachangia Afrika Kusini kupata ushindi.
Chapisho hilo la SATV.ma limedai wachambuzi wa michuano hiyo wanatilia mashaka uwepo wa Motsepe katika kila mechi za Bafana Bafana na kudai kuwa unaathiri hadi uchezeshaji wa waamuzi wa mechi.
Afrika Kusini imefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya AFCON 2023, baada ya kuwatoa Morocco hatua ya 16 bora na Cape Verde hatua ya robo fainali
Post a Comment