π™Šπ™†π™π˜Όπ™ƒ π˜Όπ™π˜Όπ™Šπ™‰π™‚π™€π™•π˜Ό π™π˜½π™π™‰π™„π™π™


 ... Katika dirisha dogo lililopita sikuandika kitu kuhusu usajili, lakini niliwaambia marafiki zangu kwenye group letu kuwa .... 


... Okrah ni usajili bora wa dirisha dogo iwapo asipopata injury. Yanga SC wameongeza idadi ya magoli na ubunifu kwenye eneo la mwisho. Akiendelea kupewa game time watu watamsahau MOLOKO aliyempisha Okrah ☑️


Namba ya viungo washambuliaji wabunifu imeongezeka hali ambayo itamfanya mwalimu awe na wigo mpana wa machaguo.


◉ π™Šπ™ π™§π™–π™ π™ˆπ™–π™œπ™žπ™˜

◉ Stephane Aziz Ki

◉ Pacome Zouzoua

◉ Maxi Nzengeli


πŸ“Œ Kama si kukosa kwa umakini kwa washambuliaji wa Yanga Okrah angeondoka na ASSISTS (4) kwenye game.


Ni Mchezo wake wa (1) kuanza katika kikosi cha Yanga, tayari ana Assists (2) 🎯🎯


Alichosema Gamondi baada ya mechi πŸ—£️


"Kuna muda huwa tunahitaji kupata mabao kupitia pembeni na leo Okrah ameonesha uwezo huo, kasi yake na uwezo wake wa kutengeneza nafasi umeongeza kitu kwenye timu... Ni mchezaji mzuri washambuliaji watatamani kucheza na winger kama yeye wakiamini pasi ya bao itakuja tu"


©️ Miguel Gamondi - Kocha Yanga

No comments