Pasi za Stars hazikuwa na Faida


 “Kuna kocha aliwai kusema takwimu ni kama mtoto wa kike aliyevaa sketi fupi, utaona baadhi ya vitu lakini haikupi nafasi ya kuona kila kitu. Umiliki wa Taifa Stars ulikuwa zaidi kwa kucheza kwa safu ya ulinzi, pasi ya hatari ni ile ya kwenda mbele na hakuna pasi zinazopigwa kwenda mbele. Congo nao walikuwa na faida ya kupata sare kwahiyo walikuwa wanatuangalia tu kwamba acha tuendelee kupiga pasi nyingi nyuma.”



“Takwimu zinaonyesha tumemiliki sana mchezo lakini kiuhalisia hakukuwa na faida ya hiyo kumiliki mpira sababu pasi zilikuwa zinapigwa sana nyuma, kitu ambacho Congo walikuwa wanahofia ni zile kona, kama ikitokea tumepiga kona alafu tungepata goli inamaana Congo waliumizwa kichwa na hilo ndiyo maana wakawa wanashambulia.”


“Kwa mtu ambaye hakuangalia msimamo, basi angejua Taifa Stars ndiyo wanahitaji sare kwavile tulivyokuwa tunacheza na kutokuweka nguvu kwenye ushambuliaji. Kitu ambacho tulifanya vizuri ni kwenye kuzuia na kutowapa nafasi ya kutengeneza mashambulizi ya hatari.”


“Nafasi zilizopatikana ni zile ambazo mchezaji mwenyewe anatakiwa kujitengenezea nafasi mwenyewe na sio nafasi zilizotengenezwa kiushambuliaji na kimfumo zaidi.”

- Amesema mchambuzi George Ambangile kupitia Wasafi FM

No comments