Naomba nisaidie nifanye nini ili kuahirisha hii harusi


 "Nimevalishwa pete lakini sijui nafanya nini na hii pete. Niko na huyu mwanaume huu ni mwaka wa tano lakini kuna mahusiano mengine ambayo niko na mwanaume mume wa mtu yeye ndiye ananihudumia kwa kila kitu.


Mimi nafanya kazi niko benki mshahara wangu kwa mwezi ni kama laki 9 hivyo siwezi kumudu mahitaji yangu kwani nyumba yenyewe tu nalipa laki tano kwa mwezi hivyo ni huyu Baba ananilipia ingawa mchumba wangu anajua kuwa ni mambo ya kazini.



Sasa huyu mchumba wangu ana miaka 35 na muda mrefu amekuwa akiniambia kuhusu kunioa namzungusha sababu ni moja, huyu baba niliyeko naye kuna nyumba ananijengea ni kubwa tu na mipango yake ni ikiisha tuhamie wote.


Si kama anamuacha mke wake hapana lakini nakuwa kama mchepuko wa kudumu kitu ambacho sina mpango nacho. Mipango yangu ni kuwa akishanimalizia kujenga naipangisha halafu anachana naye kisha namuambia huyu mwanaume wangu tuoane.


Nyumba ilikuwa iishe mwaka jana lakini kuna mambo yakatokea huko kazini kwake akaamishwa kazi hivyo sasa hivi ndiyo amerudi na ujenzi ni kama umeanza tena kwani tulishapaua tu. Mimi na mchumba wangu kila siku nimekuwa nikiahirisha lakini mwaka jana nikijua kuwa kila kitu kitakuwa tayari mwaka huu niliwaruhusu wakaja nyumbani kujitambulisha.


Wakapanga mahari na kila kitu ila pete na uchumba rasmi ilikuwa bado na mimi ndiyo nilikuwa namuambia siko tayari. Sasa baada ya huku mambo kuharibika nilimuambia tusubiri kwanza ila kilichotokea kumbe mshenga aliongea na Baba wakapanga kuhusu kuja kuleta mahari, sijakaa sawa ananiambia wameshaongea na baba hivyo mahari imeletwa na pete nimevalishwa.


Kweli sitaki kuolewa kabla ya mambo yangu hayaajakamilika shida inakuja kuwa kila kitu sasa hivi ni mshenga na Baba anataka niolewe. Nimeongea na mama kuhusu kuahirisha kwani yeye anajua kila kitu changu lakini kaongea na Baba ila hataki, ananiambia yeye kashaitwa watu wameshatoa mahari mimi si mtoto wake tena anataka niwe ameolewa."


Hali hii imenifanya kuwa na kisirani sana, najikuta namchukia mchumba wangu namkatirikia bila sababu. Ndoa ni mwezi 5 lakini sijaandaa chochote wakati Baba kashanzisha vikao ila mimi siko tayari kabisa, yaani sijui nafanya nini?


Namtukana mchumba wangu ili kuahirisha hata hadi mwakani lakini anakua mpole kitu kinanipa hasira zaidi kwani ananiambia ni paniki tu ya ndoa lakini hakuna shida. Yule Baba ndiyo kaniganda ni kama kahisi kitu kwani nikimuuliza kuhusu document za viwanja ananiambia una hataka nini nitakupa tukihamia.


Nimemvumilia sana huyu Baba si kama nampenda ili niwe na maisha mazuri, najua akisikia nimeolewa hatanipa hata shilingi mia miaka yangu yote ujana wangu utapotea bure.


Naomba nisaidie nifanye nini ili kuahirisha hii harusi, sitaki kuendelea kumtukana mchumba wangu kwani atanicha na mimi baada nampenda nina miaka 30 nikiachwa na huyu siwezi pata mwanaume mwingine nisaidie nafanya nini?"

NA MWANDISHI : IDDI MAKENGO



No comments