INONGA KUENDA FAR RABAT, JE SIMBA SC WATAWEZA KUMBAKISHA
Hapo jana tumepokea taarifa juu ya INONGA BAKA kusaini Mkataba wa awali kwaajili ya kuitumikia Far Rabat msimu ujao
Kisheria ni kwamba kama mchezaji bado ana mkataba na klabu fulani hana ruhusa ya kufanya mazungumzo na klabu nyingine ila klabu inayomuhitaji inatakiwa ifanye mazungumzo na klabu inayommiliki mchezaji husika
Lakini anaruhusiwa kufanya mazungumzo pale tu mkataba wake ukiwa umebakiza miezi michache ili kumalizika
Na Inonga tayari kafanya mazungumzo na Far Rabat ya Morocco
Hii inamaanisha Inonga Mkataba wake na Simba huenda ukaisha mwishoni mwa msimu huu, hivyo basi kazi imebaki kwa Simba
Kwakua wanahitaji kujenga timu imara cha muhimu ni kumuita mezani Inonga baada ya yeye kurejea kutoka timu ya Taifa na waongee anahitaji kiasi gani ili asaini Mkataba mpya, kwani mpaka sasa Inonga thamani yake imepanda
Wakimuongezea pesa sidhani kama Inonga ataondoka Msimbazi lakini Simba wakiwa wabahiri basi Utawala wa wa waarabu utaendelea kuzitesa timu zetu.
SIO RAHISI KUMPATA BEKI MWINGINE KAMA HENOCK INONGA BAKA 🇨🇩.
✍️ Mr_J
Post a Comment