HATARI SANA: GHANA Imebaki Jina tu..
Ghana imebakia jina tu, inasikitisha sana aisee 😢
Miaka ya nyuma ukiskia timu ya taifa ya Ghana unajua kabisa ni timu ya boli miamba kwelikweli ila kwa sasa kwisha habari yao imekuwa timu ya mabishoo tupu hawana uwezo wa ajabu uwanjani wala vipaji vya kutisha kama zamani. Timu ya taifa ya Ghana saiv mchezaji pekee wa kipaji kikubwa ni Mohamed Kudus labda kidogo na yule Semenyo
Soka la Ghana linatajwa kuporomoka kuliko udongo kule Hanang. Unaambiwa nchini Ghana mashabiki hata uwanjani kwenye ligi yao hawafiki viwanjani. Ligi imekuwa mbovu ndio maana kwa sasa tunaona hata ligi kuu ya Tanzania imekuwa kubwa kuliko ya Ghana.
Soka ni mchezo unaohitaji maendeleo endelevu uwekezaji na usimamizi mzuri ivi mmesahau Tanzania tuliwahi kuwafunga Morocco goli 3 kwa 0 uwanja wa mkapa mwaka 2013 ila miaka 10 baadae sasaiv Morocco wapo level gan?
Post a Comment