🔰 | 𝗬𝗔𝗡𝗚𝗔 𝗦𝗜𝗪𝗔𝗢𝗡𝗜 𝗥𝗢𝗕𝗢
Majibu ya mchambuzi baada ya kuulizwa, "Yanga wana nafasi ya kwenda robo fainali ? Na vipi kuhusu Simba ?"
"Kundi la Simba liko wazi japo ni ngumu kwa sababu Wydad wanazitaka points za nyumbani na ugenini. Simba anapaswa kushinda ugenini na nyumbani."
Simba imecheza vizuri na Jwaneng viwango vya wachezaji vimeimarika tangu aje Benchikha. Kundi bado liko wazi"
"Yanga kufuzu ni ngumu. Kwangu Yanga kushinda mechi ni mafanikio kwao kwa sababu mara ya mwisho kucheza group stage champions league hawakushinda mechi yoyote na walimaliza wa mwisho kwenye kundi. Kwa sasa malengo ya Yanga ni kushinda mechi, ikitokea wameenda robo fainali champions league ni bonus"
©️ Wilson Oruma
Mchambuzi wa EFM radio
.
.
𝗦𝗶𝗺𝗯𝗮 𝗸𝘄𝗲𝗻𝗱𝗮 𝗿𝗼𝗯𝗼 𝗻𝗴𝘂𝗺𝘂 :
“Nafasi ya Simba kwenda robo fainali imeanza kuwa ngumu zaidi. Simba wameambulia pointi mbili katika mechi zao mbili za mwanzo. Na sasa wana safari ya kukabiliana na Wydad pale Morocco. Mechi mbili zijazo watacheza na hawa jamaa wa Afrika Kaskazini wakianzia na pambano la ugenini ambalo litakuwa la machozi jasho na damu kwa wenyeji.
.
Tayari Wydad wamepoteza mechi mbili. Moja nyumbani dhidi ya Jwaneng nyingine wamepoteza juzi Jumamosi dhidi ya ASEC Mimosas. Pambano hili dhidi ya Simba watalitumia kwa kujaribu kuwafuta machozi mashabiki wao. Hawatataka kufungwa mechi ya pili mfululizo nyumbani, au mechi ya tatu mfululizo katika kundi. Simba wana kazi. Kama Simba wataweza kufanya vema katika mechi mbili zijazo dhidi ya Wydad, huku ASEC na Jwaneng wakipunguzana wenyewe kwa wenyewe inaweza kuwasaidia. Tatizo ni kwa Simba ipi? Hii ya Onana? Benchikha ana kazi kubwa ya kufanya. Tusubiri tuone.”
©️ Edo Kumwembe.
Mchambuzi wa kituo cha Wasafi
Sema yanga unapoanza kuwakatiaa tamaa ndo huwaa wanaamkaaa na kukuaibishaa tusubiriee game mbili zijazo tutakuwa na point 7
ReplyDelete