Mo afunguka ukweli kuhusu Sakho


 Nimeiona hii barua ya TFF, leo naomba niandike kama Shabiki tu wa Simba kuhusu hali yetu kidogo ya sasa! Ni ukweli usioficha kwamba kuna kelele nyingi zinapigwa ila haswa ni kelele tatu, ya kwanza ni DERBY bado majeraha hayajapona, kelele ya pili ni JEZI na ya tatu sasa ni DENI la mauzo ya Pape Ousmane Sakho sahau kuhusu Kocha na mambo mengine ya Posho, ambazo zote hizi kelele wanazibeba Mashabiki na ndio wao Wahanga wakuu.


Kudaiwa ama kufungiwa na FIFA sio issue kubwa ni kawaida kwa klabu kuchelewesha malipo huenda wao hawajalipwa ama structure za malipo ni instalments sometimes ni kawaida malipo kucheleweshwa kwakuwa klabu nyingi hazilipi mzigo wote mara moja, ila kwa kutambua uzito wa dirisha hili la usajili naamini Simba itachukua hatua za haraka kutatua changamoto hi, ni kawaida hata wengine walifungiwa.


VIONGOZI wetu jambo la muhimu kwasasa ni kusikiliza mitazamo yote chanya kwa maslahi ya klabu! Utetezi umekuwa mwingi na maneno

yamekuwa mengi Mashabiki wakiipambania nembo ya klabu ila sasa ni wasaa wenu wa kupush vitu vitokee, huu unyonge sio afya sana kwa ustawi wa brand ya Simba na matukio yamekuwa mengi.


Timu inapoyumba tusitafute watu wa kubeba agenda ya kusafisha, ni kama kutumia Panadol ama kujipiga ganzi ila maumivu yanasalia,

tukubaliane kupambana na Jinamizi la kweli linaloitwa UKWELI, tupigane nae kwa kurekebisha vitu! Simba kwasasa ni kamna kisiwa imejifungia kwa watu wa Bodi, ni timu kubwa sana hiyo, hakikisheni kuna ldara kadhaa wekeni watu wapush mipango ya klabu kitalaam.



Mimi kama Mwandishi naweza kuona ni sahihi kisheria kwa kinachoendelea lakini nikijifungia home kwa kinachoendelea ndani ya klabu kinaumiza na kinakatisha tamaa, lakini hii ni timu yetu naamini Simba anapaswa kuunguruma tena! Kuna Asec Mimosa hapo mbele, makelele haya sio mazuri sana wakati huu, ila tunaombea tuvuke salama.


Haya ni matokeo ya kujifungia kama kisiwa, lakini makosa yapo ili tujifunze! It will be calm after the storm In shaa Allah! Tutadharirika

Sometimes, tutaumia sometimes lakini hii ndio timu yetu na hatuna pa kwenda.


CC: Mohammed Dewji

No comments