BACCA ASAINI MKATABA NANGWANI MPAKA 2027


 Klabu ya Yanga leo imetangaza rasmi kuwa beki wake wa kati kutokea Zanzibar Ibrahim Bacca wamemuongezea Mkataba mpya hadi 2027.

Rais wa Yanga Hersi mapema leo alinukuliwa akisema kwamba wana mpango na Bacca kuhakikisha kuwa anazeekea Jangwani.

Nje ya utambulisha huo siku ya Jumamosi Desemba 2 2023 katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Yanga vs Al Ahly itakuwa ni Bacca Day ambapo mashabiki wa Yanga watatakiwa kwenda uwanjani wakiwa wamevalia msuli.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Bacca alijiunga na Yanga January 14 2022 akitokea timu ya jeshi Zanzibar ya KMKM ambapo alijiunga na Yanga baada ya kukubaliwa likizo ya bila malipo hivyo akistaafu soka atarudi kuendelea na kazi yake ya uaskari.

No comments