Simba Out, lakini Simba ni Darasa kwa Yanga
NI FOOTBALL ...! FT: Al Ahly 1-1 Simba SC ( Agg: 3-3 )
✍🏻Tangu ya filimbi ya kwanza ulikuwa unajua nini makocha wote wawili wanataka katika mechi : Al Ahly alitaka kufunga goli ili awe na mtaji mwingine mkononi wakati Simba hawakutaka kuifungua mechi kwa kuruhusu magoli zaidi ndio maana walikuwa nyuma muda mrefu
1: Nafikiri kocha wa Al Ahly atakuwa anawauliza wachezaji wake hii mechi imeishaje 1-1 ? Kwa nyakati nzuri za kutengeneza au kufunga magoli walizopata ? Msingi wa Al Ahly ulikuwa nini ?
1: Attia kwenye kiungo ndio alikuwa mchezaji mwenye ufunguo wa Al Ahly , kivipi ?
2: Anakuwa kwenye positions ambazo anahakikisha ana intercept mipira na pia kushinda mipira mingi ya pili , dhumuni ? Ni kudumisha mashambulizi .
3: Jinsi El Shahat na Maâloul pamoja na Afsha walivyokuwa wana combine sana upande wao wa kushoto na kulia kwa Simba ilikuwa kazi ngumu kwa Kapombe hasa ukizingatia winga wake alikuwa wanachelewa kurudi nyuma .
✍🏻Simba SC kipindi cha kwanza ni kama vile kuna nyakati wachezaji walikuwa wabaufanya mpira kama moto , na wengine wanajificha pale ambapo mabeki wao wana mpira matokeo yake ilikuwa rahisi kwa Al Ahly kufanya counter pressing haraka kurudisha mpira kwenye himaya yao
1: Viungo washambuliaji wa Simba mipira ikifika kwao inapotea kirahisi badala ya kukaa nayo
2: Mabeki wana mali mguuni lakini hawana options za kutosha za kupasia
3: Viungo wa ulinzi wanaogopa kusogea juu kwa hofu ya turn overs na kumuacha Afsha nyuma yao .
✍🏻Ni mpaka pale Simba walipokuwa wanatafuta goli la pili baada ya Al Ahly kusawazisha , wingbacks wakaanza kusogea juu huku nyuma wanabaki mabeki watatu maana yake waliwalazimisha Al Ahly kukabia chini zaidi na kusubiria counter attacks
NOTE
1: Kwenye football , kushambulia pamoja na kuzuia pamoja ... winga wa kulia wa Simba ali switch off katika wakati muhimu sana . Huwezi kumpa space kama ile Maâloul.
2: Attia kiungo kisheti , anafanya mambo kuwa rahisi
3: Recovering za Che Malone na blocks zake 🔥
4: Kuna nyakati Simba walitembea sana na bahati zao , aina ya nafasi na actions za kusababisha magoli ambazo Al Ahly walikuwa wanapata ..🤔
5: Kahraba movement yake 🔥
Post a Comment