Mendy amekana tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia alizokuwa akituhumiwa nazo.
Beki wa Manchester City na staa wa kimataifa wa Ufaransa 🇫🇷 Benjamin Mendy amekana tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia alizokuwa akituhumiwa nazo.
Mendy alikuwepo katika Mahakama ya Chester Crown wakati kesi yake ilipokuwa ikisilizwa. Awali Mendy alikana kesi saba za unyanyasaji wa kijinsia kabla ya kupenyezewa mashataka mengine matatu, hata hivyo aliyakana yote mahakamani.
Mendy, 28, alishtakiwa kwa makosa ya kuwanyanyasa kijinsia wanawake saba mwaka 2018 na Agosti mwaka jana. Beki huyo alitakiwa kusimama kizimbani kusikiliza kesi yake inayosimamiwa na Louis Saha Matturie.
Mendy alianza kuichezea Man City tangu mwaka 2017 alipojiunga akitokea Monaco kwa kitita cha Pauni 52 milioni. Kwa sasa yupo nje kwa dhamana wakati kesi yake ikiendelea kuunguruma mahakamani.
Wakati huohuo huenda wachezaji wa Man City, Jack Grealish, John Stones, Riyad Mahrez, na Kyle Walker wakaitwa na mahakama kama mashahidi wa Mendy kwenye kesi hiyo itakaposikilizwa tena.
Post a Comment